Breaking News
Loading...

Advert

Thursday, March 31, 2016

Rwanda imemfunga jela askari aliyekuwa kamanda mkuu wa kikosi cha kumlinda Rais kagame miaka 21.

Aliyekuwa kamanda mkuu wa kikosi cha ulinzi
wa Rais Paul Kagame, Kanali Tom Byabagamba,
amehukumiwa kifungo cha miaka 21 jela na
kuvuliwa cheo chake baada ya kupatikana na
hatia ya kuharibia sifa nchi hiyo na kuhamasisha
wananchi kupinga utawala.
Kesi hiyo ilimhusisha pia brigedia jenerali
mstaafu Frank Rusagara ambaye naye
amepatikana na hatia na kuhukumiwa miaka 20
jela.
Maafisa hao wa jeshi wamepinga hukumu hiyo
wakisema mashtaka dhidi yao yalichochewa
kisiasa.
Mahakama imeunga mkono hoja za upande wa
mwendesha mashtaka kwamba mlinzi wa muda
mrefu wa Rais Kagame, Kanali Byabagamba,
alihusika na makosa matatu ambayo ni kueneza
kampeni za chuki dhidi ya utawala ambazo
zingesababisha wananchi kugoma dhidi ya
serikali ya nchi hiyo na kutoheshimu bendera ya
nchi hiyo.
Brigedia jenerali mstaafu Frank Rusagara naye
amepatikana na makosa kama hayo pamoja na
kosa la kumiliki silaha kinyume cha sheria.
Awali alikiri kumiliki bastola mbili alizopewa kama
zawadi na nchi za Afrika Kusini na Israel, wakati
alipokuwa afisa mkuu anayehusika na ununuzi wa
silaha katika wizara ya ulinzi ya Rwanda.
Maafisa hao wamekata rufaa baada ya
mahakama kutangaza hukumu hiyo

0 comments :

Post a Comment

Back To Top