Rushwa mahakama ya kisutu katika kutoa haki Takukuru wailalamikia.soma zaid.
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar
es salaam imelalamikiwa kuwa inaendekeza
vitendo vya rushwa katika utoaji haki, anaandika
Faki Sosi.
❝
Akizungumza baada ya kuachiliwa huru
Williamu Mhando aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu
wa Tanesco, Leornaed Swai Mwanasheria wa
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa
(Takukuru) amesema kuwa rushwa katika
mahakama ya Kisutu inatisha.
Swai ametoa tuhuma hizo baada ya Hakim
Hellen Liwa kusoma hukumu kwa niaba ya Kyey
Rusema ambapo iliamriwa kuwa mahakama
imemuona Mhando hana hatia.
Mahakamaa imeeleza kuwa hakuna ushahidi
ilionyesha kuwa Mhando alitumia madaraka yake
vibaya kutokana na mkataba wa Tanesco kuipa
zabuni ya mkewe kampuni ya Santa Clara, na pia
yeye hakuhusika kwenye kutoa zabuni kwa kuwa
zabuni hutelewa na bodi ya zabuni.
Mahakama imeeleza kuwa hakuna ushahidi wa
yeye kujua kuwa Santa Clara ni kampuni ya mke
na watoto wake kwani inwezekana mke akawa
na akaunti benki mumewe asijue.
Mshtakiwa namba mbili Eva Mhando ameonekana
hana hatia kutokana na hakuna ushahidi
ulionyesha kuwa ameghushi nyaraka.
Kesi ilikvyokuwa
Mhando na mkewe walikabiliwa na mashitaka ya
matumizi mabaya ya madaraka, kughushi na
kujipatia Sh. Milioni 31.7 kwa njia ya
udanganyifu.
Kadhalika, Mhando alikabiliwa na matumizi
mabaya ya madaraka kwa kuipa zabuni Kampuni
ya Santa Clara Supplies Ltd, huku akijua ana
maslahi nayo na kwamba anaimiliki yeye, mke na
watoto wake.
Mwendesha Mashitaka wa Taasisi wa Kuzuia na
Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai
aliwasomea mashitaka hayo mbele ya Hakimu
Mkazi Frank Moshi na kwamba washitakiwa kati
ya Aprili Mosi na Desemba 31, mwaka 2011
katika ofisi za Makao Makuu ya Tanesco jijini
Dar es Salaam, Mhando akiwa kama Mkurugenzi
wa shirika hilo, alitumia vibaya mdaraka yake
kwa kujiingizia maslahi yake binafsi
Mshitakiwa aliipa zabuni kampuni inayongozwa
mke wake, Eva na watoto wake, ya kusambaza
vifaa vya Tanesco vyenye thamani ya Sh. Milioni
884.5 na kuisababishia kampuni hiyo kupata
faida ya Sh. 31,747,000 kinyume cha sheria .
Katika shitaka la pili, ilidaiwa kuwa kati ya
Januari 6 na Julai 30, 2011, mahali
pasipofahamika, jijini Dar es Salaam, Eva
alighushi taarifa ya ukaguzi wa fedha ya
Kampuni ya Santa Clara Ltd, akionyesha kwamba
imekaguliwa na Finx Capital House Desemba
mwaka 2010.
Katika shitaka la tatu, 9Agosti, mwaka 2011 jijini
Dar es Salaam, mshtakiwa Eva alighushi nyaraka
za umiliki wa hisa kutoka Santa Clara Supplies
Ltd kwenda Eveta John Shing’oma huku akijua
siyo kweli.
Shitaka la nne, 5 Agosti, mwaka 2011 katika ofisi
za Makao Makuu ya Tanesco, jijini, mshtakiwa
Eva aliwasilisha nyaraka za manunuzi za
kughushi akionyesha kwamba taarifa hiyo
imeandaliwa na Finx Capital House huku akijua
siyo kweli.
Katika shitaka la tano, ilidaiwa kuwa kati ya Aprili
na Oktoba, mwaka 2011 jijini Dar es Salaam, Eva
akiwa kama Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya
Santa Clara Limited kwa nia ovu, alijipatia faida
ya Sh. 31.7 milioni kutoka Tanesco baada ya
kuwasilisha nyaraka za ukaguzi za kughushi.
Shitaka la sita, 17 Oktoba , mwaka 2011 katika
ofisi za Tanesco, mshtakiwa wa tatu hadi wa
tano, Mchalange, Misidai na Kisinga wakiwa
watumishi wa shirika hilo, walipokea nyaraka za
kughushi na kusababisha Kampuni ya Santa Clara
Supplies Limited kupewa mkataba wa kusambaza
vifaa vya ofisini. Ilidaiwa kuwa mkataba huo
ulisababisha kampuni hiyo kupata mkataba wa
zabuni ya kusambaza vifaa vya Sh. 884.5 milioni
na kupata faida ya Sh. 31.5 milioni.
1.chanzo mwanahalisonline.
0 comments :
Post a Comment