Hizi ni kashfa tatu zinazoikumba hospital ya mhimbil.soma zaid
Awali, Meneja wa Kitengo cha Mawasiliano cha
MNH, Aminiel Aligaesha akizungumzia matukio
hayo alisema Muhimbili haijawahi kufanya
upasuaji wowote kimakosa
Kwa ufupi
1. Kuchanganya maiti
2. Kupasuliwa mguu badala ya kichwa na
kichwa badala ya mguu
3. Sindano yasababisha mtindio
By Mwandishi Wetu, Mwananchi ;
mwananchipapers@mwananchi.co.tz
Dar es Salaam. Hospitali ya Taifa Muhimbili
(MNH) imejikuta ikipatwa na kashfa nzito tatu
kutokana na uzembe wa watendaji wake, haswa
hivi karibuni baada ya kutoa mwili wa marehemu
kwa watu tofauti ambao nao bila ya kujua,
waliusafirisha na kuuzika Usangi, Mwanga
mkoani Kilimanjaro.
Hiyo ni kashfa ya tatu kuikumba hospitali hiyo
katika matukio tofauti baada ya mwaka 2007,
mgonjwa mmoja kupasuliwa mguu badala ya
kichwa na mwingine kichwa badala ya mguu
katika Taasisi ya Tiba za Mifupa Muhimbili (MOI)
.
Nyingine ni ile ya mtoto Imrani Mwerangi (3)
ambaye hivi sasa ni marehemu aliyefikishwa
katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Julai 28, 2011
kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa nyama
zilizokuwa puani, lakini akadungwa sindano
iliyomletea matatizo.
Julai 29, 2011, mtoto huyo aliyesajiliwa kwa
jalada IP.No. A586301 aliingizwa katika chumba
cha upasuaji mdogo wa nyama za puani na kabla
ya upasuaji huo, alidungwa sindano ya usingizi
ambayo ndiyo iliyomsababishia matatizo ya
mtindio wa ubongo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Muhimbili, Profesa
Lawrence Museru akizungumzia matukio hayo
alisema kuwa kila tukio lina ufafanuzi wake.
Kuhusu mtoto Imran kuchomwa sindano
iliyomletea madhara alisema lile halikuwa kosa la
kibinadamu bali ni matokeo ya sindano jambo
ambalo linaweza kumtokea yeyote.
“Hata huko Marekani matukio kama haya
yanatokea pale sindano za anesthesia zinapoleta
madhara lakini si kwa uzembe,”alisema.
Kadhalika Profesa Museru alizungumzia suala la
maiti kubadilishwa MNH na kusema kuwa
uongozi wa hospitali unafanya uchunguzi kujua
kosa lilikuwa la uzembe au bahati mbaya.
‘Kwa sababu hatujui ilikuwaje mpaka mhudumu
akakosea kutoa mwili na kwa nini akosee, kwa
siku pale mochwari tunatoa maiti zaidi ya 30
sasa ndiyo tujue kwa nini hiyo ilikosewa,”alisema
Awali, Meneja wa Kitengo cha Mawasiliano cha
MNH, Aminiel Aligaesha akizungumzia matukio
hayo alisema Muhimbili haijawahi kufanya
upasuaji wowote kimakosa.
“Hili lililotokea juzi lazima tukiri upungufu
uliojitokeza na tumeongeza internal controls za
kutosha kuhakikisha halitokei tena. Moja ikiwa ni
kila mtu kwa nafasi yake anatimiza wajibu wake
ipasavyo,”alieleza Aligaesha katika ujumbe wake
kwa gazeti hili.
Kuchanganya maiti
Wiki iliyopita hospitali hiyo kwa kushirikiana na
Jeshi la Polisi, walilazimika kufukua maiti ya
Janeth Bambalawe (65), kuirejesha Dar es
Salaam ili ikabidhiwe kwa wahusika. Hiyo ni
baada ya kuachwa kwa makosa maiti ya Amina
Msangi (79) katika chumba cha kuhifadhia maiti
cha MNH.
Sintofahamu hiyo ilitokea Aprili 12, asubuhi
baada ya ndugu wa Janeth, kufika mochwari
Muhimbili ili kuuchukua mwili wa marehemu huyo
kwa ajili ya maziko katika makaburi ya Kipunguni,
Ukonga na kuukosa.
Akizungumzia mkasa huo Mkurugenzi wa
Huduma za Tiba Shirikishi MNH, Dk Praxeda
Ogweyo alisema ndugu wa Amina ambaye
alifariki dunia Aprili 8, hawakuukagua mwili wa
marehemu baada ya kupewa na badala yake
waliondoka na mwili wa Janeth.
Alisema marehemu Amina aliyefikishwa
hospitalini hapo kwa rufaa akitokea Temeke Aprili
6 na kulazwa wodi namba 12 katika jengo la
Kibasila, alihifadhiwa ndani ya jokofu moja na
Janeth ambaye alifikishwa hapo akitokea
Hospitali ya Amana Aprili 4 na kulazwa wodi
namba mbili jengo la Mwaisela. Naye pia alifariki
dunia Aprili 8.
“Wote walifariki siku moja, wakahifadhiwa katika
jokofu moja kwa hiyo mtumishi wa mochwari
alipokwenda kuutoa mwili alichanganya badala
ya kuwapatia mwili wa Amina, akawapa ule wa
Janet na ndugu nao hawakushiriki kikamilifu
kukagua,” alisema Dk Ogweyo.
Alisema kwa kutambua kosa hilo, Muhimbili ilitoa
gari la wagonjwa na wafanyakazi wawili kwa ajili
ya kuupeleka mwili wa Amina, Usangi kwa ajili ya
mazishi na kuurejesha Dar es Salaam ule wa
Janeth ambao ulirejeshwa na kuzikwa siku
hiyohiyo.
Mbali na hatua hiyo, Dk Ogweyo alisema
mtumishi aliyefanya kosa hilo amesimamishwa
kazi kupisha uchunguzi.
Akielezea hali ilivyokuwa mtoto wa marehemu
Janeth, Peter Mkude alisema walipofika
Muhimbili aliingia na kuonyeshwa mwili wa mama
yake ambao hakuutambua, akatoka na aliporudi
mara ya pili aliongozana na mama zake wadogo
wawili na dada yake, lakini pia hawakuutambua.
Kuona hivyo walikwenda katika ofisi za utawala
ambako waliongozwa kwa mwanasheria ambaye
baada ya maelezo, waliongozana naye hadi
mochwari na baada ya kuthibitisha kwamba mwili
umekosekana, walikwenda Kituo Kikuu cha Polisi
ambako waliandikisha maelezo na kupewa ahadi
ya kurejeshewa mwili wa ndugu yao.
“Walitwambia kwamba wataufukua na kufikia
Aprili 13, tutakuwa tumeupata, tumepanga kuzika
siku hiyohiyo katika makaburi ya Kipunguni
Mashariki, Ukonga saa 10 jioni,” alisema Mkude.
Kupasuliwa mguu badala ya kichwa na kichwa
badala ya mguu
Novemba mwaka 2007 katika Taasisi ya Tiba za
Mifupa Muhimbili (Moi), mgonjwa Emmanuel
Mgaya alifanyiwa upasuaji wa mguu badala ya
kichwa na Emmanuel Didas kufanyiwa upasuaji
wa kichwa badala ya mguu.
Mgaya alilazwa katika wodi ya Sewahaji namba
17 baada ya kufanyiwa upasuaji huo, na Didas
alilazwa katika wodi ya wagonjwa wanaohitaji
uangaalizi wa karibu (ICU) baada ya kufanyiwa
upasuaji wa kichwa badala ya mguu.
Didas alifungua kesi mahakama kuu akidai fidia
ya Sh800 milioni kutokana na athari alizozipata,
lakini mahakama hiyo ilitaka kesi hiyo ipelekwe
kwenye usuluhishi.
Sindano yasababisha mtindio
Mtoto Imrani Mwerangi (3) ambaye hivi sasa ni
marehemu alipelekwa nchini India kwa matibabu
baada ya kudungwa sindano iliyomsababishia
mtindio wa ubongo katika Hospitali ya Muhimbili.
Imrani alipelekwa nchini India na Serikali baada
ya kulazwa ICU ya Muhimbili tangu Julai 28,
2011.
Taarifa zilieleza kuwa madaktari waliomhudumia
walisema mtoto huyo angeendelea kutegemea
matibabu katika maisha yake yote.
Kwa mara ya kwanza mtoto huyo alifikishwa
katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Julai 28, 2011
kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa nyama
zilizokuwa puani ambapo alipokewa na
kufunguliwa jalada IP.No.A586301.
Julai 29, 2011 mtoto huyo aliingizwa katika
chumba cha upasuaji mdogo wa nyama za puani,
lakini kabla ya upasuaji huo alidungwa sindano ya
usingizi ambayo ndiyo iliyomsababishia matatizo
ya mtindio wa ubongo.
Hadi umauti unamkuta Imrani mwaka jana
alikuwa katika matibabu nchini India, na mwili
wake ulizikwa eneo la Mdaula mkoani Pwanichanzo mwananch.
0 comments :
Post a Comment