Home
Unlabelled
Hivi inawezekana masikini akaogota fedha ya tajili na kumludishia?soma kisa hichi.
Hivi inawezekana masikini akaogota fedha ya tajili na kumludishia?soma kisa hichi.
Kuna siku nilikuwa maeneo ya Mjini kati (City Center), nikaipenda suruali moja ya shilingi 15,000/= na pesa sikuwa nayo ikabidi niende kutoa kwenye ATM ya Postal.
Nimefika pale sikukuta mtu hivyo niliingia moja kwa moja, nimefika mle ndani nikakuta Pesa Kibao zimemwagika pale kwenye kitundu cha kutolea pesa, ATM Card ilikuwepo pale imetokezea na Pembeni kulikuwa na Pochi ya Kike iliyoonekana kutuna vilivyo.
Kwa woga mimi huku nikitetemeka mapigo ya moyo yakiwa yameongezeka nikatizama nyuma yangu sikuona mtu, nikachukua zile Pesa harakaharaka, ATM na ile pochi.
Ile natoka nje kuna dada mmoja alikuwa anakuja kwa kasi maeneo yale nikapata uoga nikamuuliza “Samahani dada, kuna kitu umesahau humu”, yule dada hakunijibu kitu kaingia kwenye chumba cha ATM akachomeka Kadi kutoa hela mi nikaondoka zangu fasta kuelekea home.
Nimefika home nikajifungia ndani na kuzibwaga zile pesa kitandani, nikafungua wallet nikakuta imejaa dollar, Vipodozi, iphone na ki-Nokia kidogo cha tochi, ATM Card mbili za Benki tofauti ambazo zilikuwa zimezungushiwa karatasi iliyokuwa na namba za siri za ATM zote, moyo ukanilipuka paaaa!!! Nikaona bora Nipumzike kwanza kitandani!!
Muda si mrefu ile iphone ikaanza kuita, nilipoangalia halikutokea jina nikaona bora nipokee nimsikilize anasemaje, ilikuwa sauti ya kike iliyoongea kwa huzuni kwa kubembeleza huku akilia na alijitambulisha vizuri kuwa ile mali ni ya kwake! Huruma ilinijia nikamwelekeza nilipo aje kuchukua...
Hakuchukua muda akawa amefika nami nikamkabidhi vitu vyote naye akavihakiki na kukuta viko sana: Milioni 3 za Kibongo na Dollar 500. Dada kanishukuru na kunipa ile Millioni 3 ya kibongo mi nikazikataa kwasababu ni mali yake na alizisahau tu.
Alinitoa hofu kwa kunisihi nichukue tu, mi kama binadamu mwenyezi Mungu atanilipa, nikakataa... Mwishowe akaomba namba yangu na kuondoka zake, akawa ameniacha ndani huku njaa sasa nikaanza kuisikia, nilikuwa na buku mbili nikaenda kula viepe kavu na soda nikawa powa.
Sasa jana kanipigia simu kuwa anakuja nimsubiri, dakika tano tu akanipigia tena kuwa ameshafika yupo nje yupo ndani ya Prado mpyaa nikaingia tukaondoka akaenda kunionyesha kwake kisha tukaelekea kwenye nyumba nyingine iliyokuwa ndo imekamilika kujengwa akaniambia hii itakuwa yako akanikabidhi baadhi ya nyaraka na funguo zote sikuamini...!!
Akanisindikiza kwangu, kufika home ananiambia hiyo gari (Prado) nayo ananiachia ni kwa mema tu niliyomfanyia, ndani ya ile gari kulikuwa na brifcase iliyokuwa na pesa akaniambia pia hii pesa itakuwa yako ya kuanzia maisha, na kumbe yule dada alikuwa kanipenda akanikumbatia kwa nguvu nikiwa pale kwenye seat oooh!! umasikini baibai...
Akiwa kanikumbatia akihema kwa kasi juu ya kifua changu nikahisi mtu akinishika begani na kuniita kwa sauti.
“Anko ankoo we ankoo... amka rafiki yako Salim anakuita!!!”.
“ALIKUWA MTOTO WA SISTA ALIKUWA ANANIAMSHA !!”.
Kumbe muda wote nilikuwa nikiota Dah...!!
0 comments :
Post a Comment