Breaking News
Loading...

Advert

Thursday, May 12, 2016

Rais maguful alikuwa kivutio jana nchini uganda akiwa kwenye sherehe za kuapishwa kwa yoweri msevini.

RAIS John Magufuli jana alikuwa kivutio kwa
maelfu ya wananchi waliohudhuria sherehe za
kuapishwa kwa Rais Yoweri Museveni wa
Uganda.
Wananchi walilipuka kwa furaha baada kiongozi
huyo wa Uganda kumtambulisha Rais Magufuli.
Rais Museveni aliapishwa kuwa Rais wa Uganda
kwa kipindi kingine cha miaka mitano katika halfa
iliyohudhuriwa na viongozi wengi wa mataifa
mbalimbali.
Tukio hilo lilirushwa moja kwa moja na vituo vya
televisheni vya ndani ya nchi na vya kimataifa.
Alipofika jukwaani, Rais Museveni alianza
kuwatambulisha wakuu na marais wa nchi
mbalimbali waliofika katika sherehe hiyo ikiwa ni
muda mfupi tangu alipoapishwa.
Mara alipotaja jina la Rais Magufuli, umati
ulirindima kwa makofi, shangwe na vigelegele,
hatua iliyofuatiwa na Rais Magufuli kusimama na
kuwapungia mkono wananchi hao.
Rais Magufuli ameibuka kuwa kiongozi maarufu
katika nchi zinazounda Jumuiya ya Afrika
Mashariki (EAC), kutokana na hatua mbalimbali
anazoendelea kuzichukua katika uendeshaji wa
serikali yake, ikiwa ni pamoja na vita dhidi ya
rushwa na ufisadi, tangu alipoingia madarakani
mwishoni mwa mwaka jana.
Akiondoka katika Viwanja vya Uhuru vya Kololo
ilipofanyika sherehe hiyo, waandishi wa habari
walijaribu bila mafanikio kutaka kufanya naye
mahojiano, lakini Rais Magufuli hakupata muda
wa kutosha wa kuzungumza nao.
Akiwa amefuatana na ujumbe wa watu
wachache, Rais Magufuli aliwasili nchini hapa
Jumatano akitokea Arusha, akitumia ndege
maalumu ya Rais.
Aliwasili Kampala ikiwa ni safari yake ya pili nje
ya Tanzania, tangu alipoapishwa kushika wadhifa
wa urais baada ya kushinda Uchaguzi Mkuu wa
mwishoni mwa mwaka jana.
Safari yake ya kwanza ilikuwa ni katika nchi ya
Rwanda. Mapema, Rais Museveni alisaini kiapo
cha uaminifu ili kulitumikia taifa hilo kwa mara
nyingine, na kukabidhiwa zana za kufanyia kazi
na Jaji Mkuu wa Uganda, Bart Katureebe.
Wakuu na marais wa nchi mbalimbali
waliohudhuria sherehe hizo, nchi zao zikiwa
kwenye mabano ni: Rais Uhuru Kenyatta (Kenya),
Rais Omar al-Bashir (Sudan), Rais Salva Kiir
(Sudan Kusini), Rais Robert Mugabe (Zimbabwe),
Rais Jacob Zuma (Afrika Kusini) na Rais
Mahamadou Issoufou (Niger).
Pia marais wastaafu wa Tanzania Ali Hassan
Mwinyi na Jakaya Kikwete walihudhuria. Marais
wengine walioonekana kuvuta hisia za wananchi
wengi na kushangiliwa kwa nguvu ni Kenyatta na
Omar al-Bashir.
Akimtambulisha Rais Al-Bashir, Rais Museveni
alisema Uganda imepuuza amri ya Mahakama ya
Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) ya kutaka
Rais Al-Bashir kukamatwa.
Alisema “ Tumeamua kupuuza agizo hilo kwa
sababu awali wakati Mahakama hii inaundwa,
tulidhani ilikuwa makini lakini baadaye
tukagundua ipo kwa ajili ya watu wasio na hatia.”
Rais Museveni aliibuka mshindi katika Uchaguzi
Mkuu uliofanyika Februari mwaka huu kwa
kupata asilimia 60.75 ya kura zote.
Alifuatiwa na mpinzani wake wa karibu, Dk Kizza
Besigye wa Chama cha Forum for Democratic
Change (FDC) aliyepata asilimia 35.37 ya kura,
huku Waziri Mkuu wa zamani, Amama Mbabazi,
ambaye alipinga mahakamani ushindi wa Rais
Museveni na kushindwa katika kesi hiyo alipata
kura asilimia 1.43.
Rais Museveni, ambaye ni Mwenyekiti wa Chama
tawala cha NRM, amekuwa madarakani tangu
mwaka 1986.chanzo habar leo

0 comments :

Post a Comment

Back To Top