Breaking News
Loading...

Advert

Friday, May 13, 2016

Serikal ilitumia sh.bilion32 kupeleka wagonjwa nje ya nchi mwaka 2012-2015.soma zaid.


Bunge la 11, mkutano wa 3, kikao cha 19
Maswali na majibu
Nape Nnauye: Kwa sasa ni hotuba ya
bajeti ya wizara ya Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo na pamoja na mambo
mengine waziri wa wizara hiyo, Nape
Nnauye ameliomba bunge kumuidhinishia
shilingi bilioni 20.3 na kati ya hizo bilioni
17 kwa ajili ya matumizi ya kawaida,
mishahara na mengineyo.
======
Swali: Je serikali ina mpango gani
kuhakikisha hakuna mwanafunzi anayekaa
chini hasa katika halmashauri ya
manispaa ya Ilemela?
Majibu: Serikali imetenga shilingi milioni
228.5 kushughuikia tatizo hilo. Vijana
wanahamasishwa kujiunga katika vikundi
vya ujasiriamali hasa katika useremala ili
kutumia fursa hii kujikwamua kiuchumi.
Swali: Serikali imetumia kiasi gani cha
fedha kupeleka wagonjwa nje ya nchi
mpaka mwaka 2015?
Majibu: Zaidi ya shilingi bilioni 32
zilitumika kwa kipindi mwaka 2012 hadi
2015, takwimu za nyuma zaidi
zitakabidhiwa punde zikikamilika.
Aidha serikali inaendelea kuleta majopo
ya madaktari kutoa tiba kutoka nje ya
nchi. Serikali inatarajia kuanza
kugharamia vipimo ambavyo ni ghali
katika hospitali kubwa hapa nchini
ikiwemo chemotherapy.
Swali: Serikali ina mpango gani
kuhakikisha upatikanaji wa dawa za
kisukari ili kuhakikisha waathirika wa
kipato cha chini waweze kuhudumiwa?
Majibu: Moja ya ongezeko la magonjwa
nchini. Kisukari kinasababishwa sana na
kutokufanya mazoezi. Dawa za kisukari
zinapatikana na katika ngazi za wilaya.
Aidha serikali itaanza kutoa huduma hizo
katika zahanati punde baada ya
wahudumu kupatiwa mafuzo. Serikali
itaendelea kuhakikisha dawa za ugonjwa
huu unapatikana na pia itaendelea kutoa
elimu ya aina ya vyakula vitakafaa kuliwa.
Swali: Je Serikali inawachukua hatua gani
juu ya ukiukwaji wa maadili ya utumishi
wa umma katika jeshi la polisi?
Majibu: Jeshi linawashughuliki kwa
kuwachukua hatua, mpaka sasa askari 19
washachukuliwa hatua za kisheria.
Serikali imesitisha utoaji wa ajira kwa
jeshi hilo ili kuweza kufanya uhakiki wa
askari hao.
Swali: Je serikali inatoa kauli gani kwa
pembejeo za kilimo kuwa hazitoshi katika
mkoa wa Ruvuma?
Majibu: Serikali inaangalia upya utaratibu
wa kutoa ruzuku bila kujali makundi na
punde ukikamilika uma utajulishwa, kodi
za excise duties zimefutwa za pembejeo
zinazotoka nje. Serikali inaangalia
uwezekano wa kuondoa tozo katika
pembejeo za kilimo zinazozalishwa nchini.
Serikali piaa imewekeza katika utafiti wa
mbegu kuhakikisha mbegu bora
zinapatikana.
Swali: Ni lini Serikali itajenga barabara ya
Maswa Mjini kuanzia Njiapanda hadi
Mwabuki kwa kiwango cha lami?
Majibu: Katika bajeti ya mwaka 2016/17
serikali imetengewa milioni 200 kwa ajili
ya kufanyia matengenezo barabara hiyo.
Swali: Je ni lini serikali itafufua barabara
ya mkoa wa Mbeya kwenda Kasanga port
na kununua Kivuko cha mto Kalambo?
Majibu: Serikali inawaasa watumiaji wa
barabara hiyo kutumia barabara ya Mbeya
->Tunduma ->Sumbawanga. Maombi
maalum ya kufufua barabara hiyo
yatumwe wizarani kupitia ngazi ya wilaya
na mkoa.
Aidha serikali imejipanga kutekeleza ahadi
zote za Mh rais katika kipindi cha
kampeni zake awamu kwa awamu.
Swali: Bunge liliridhia nyumba za NHC
zilizowekwa katika kundi A ziuzwe, kundi
B zipangishwe na kundi C zitengenezwe,
je serikali inatoa kauli gani?
Majibu: Nyumba hizo hazitauzwa na
ifahamike hivyo serikali haina mpango wa
kuziuza. Serikali inajikita kuzikarabati
nyumba hizo na kuzipangisha upya.
Serikali inafanya uhakiki kujua wapangaji
wanaopangisha nyumba za NHC baada ya
kupangishiwa na shirika.chanzo jamii forums.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top