Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, May 11, 2016

Kuflashi simu ni kosa la kukutia hatiani nani kasema ?zoma zaid.

Serikali imewataka wauzaji wa vifaa vya
mawasiliano vya mkononi (mobile
devices) kuacha mara moja tabia ya
kubadilisha namba tambulishi (‘kuflash’)
za vifaa hivyo kwani watakabiliwa na
kifungo kisichopungua miaka 10 au faini
isiyopungua Sh. milioni 30 au vyote viwili.
Kauli hiyo imetolewa na Meneja
Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania (TCRA) Bw. Innocent Mungy
wakati wa mkutano na waandishi wa
habari leo jijini Dar es salaam.
“Namba tambulishi (IMEI) za vifaa vyote
vya mawasiliano ya mkononi ambavyo
vimeibiwa,vimeharibika,kupotea au
visivyokidhi viwango vya matumizi katika
soko la mawasiliano havitaruhusiwa
kuunganishwa kwenye mitandao ya watoa
huduma ifikapo tarehe 16 June 2016,
"alisema Mungy.
Akizungumzia kampeni ya kuelimisha
umma kuhusu matumizi ya simu zote
zisizokidhi viwango, Mungy alibainisha
kuwa idadi ya simu hizo imeshuka
kutokana na elimu ambayo wameitoa
katika mikoa mbalimbali hapa nchini.
Alisema lengo la elimu hiyo kwa umma ni
kujenga uwezo kwa wananchi kutambua
simu zisizokidhi vigezo kabla ya kufika
ukomo wa matumizi ya simu bandia
nchini.
Mungy alifafanua kuwa uchambuzi wa
IMEI unaonyesha kuwa hadi
Februari,2016 idadi ya namba tambulishi
ambazo zilikuwa hazina viwango zilikuwa
sawa na asilimia tatu ambapo namba
tambulishi ambazo zimenakiliwa zilikuwa
sawa na asilimia 18 na simu halisi
zilikuwa sawa na asilimia 79.
“Kwa mwezi Machi 2016 ulionyesha kuwa
Idadi ya namba tambulishi ambazo hazina
viwango ni asilimia nne, na idadi ya zile
zilizonakiliwa zilikuwa sawa na asilimia
13 ambapo uchambuzi huu umehusisha
taarifa za kampuni zote za simu nchini,’’.
alifafanua Mungy.
Aliongeza kuwa matokeo hayo mazuri ni
matunda ya ushirikiano mzuri uliopo kati
ya mamlaka hiyo, Shirika la Viwango
Tanzania (TBS),Tume ya Ushindani (FCC)
,kampuni za simu, pamoja na wadau
wengine katika kuelimisha umma juu ya
uhakiki wa simu walizonazo ikiwa ni
pamoja na mambo muhimu ya kuzingatia
wakati wa kununua simu ikiwemo
kuzihakiki ubora wake.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa
Kituo cha Usimamizi wa Mawasiliano wa
Mamlaka hiyo, Injinia Gabriel Mruma
amesema kuwa ni vyema Watanzania
wakajenga utamaduni wa kununua simu
zenye ubora kuepuka usumbufu wakati
Tanzania inapoelekea ukomo wa matumizi
ya simu bandia.
TCRA ina dhamana ya kusimamia
shughuli za mawasiliano ya Kielektroniki
na Posta hapa nchini.
Kuwepo kwa Sheria ya Mawasiliano ya
Kielektroniki na Posta (EPOCA) ya mwaka
2010 na kanuni zake za mwaka 2011
kumewezesha kutekelezwa kwa mfumo wa
rajisi ya namba za utambulisho wa vifaa
vya mawasiliano vya mkononi.
Mfumo huu wa kielektroniki ulizinduliwa
tarehe 17, Desemba 2015 na unahifadhi
kumbukumbu za namba tambulishi za
vifaa vya mawasiliano vya mkononi kwa
lengo la kufuatilia namba tambulishi za
vifaa vilivyoibiwa,kuharibika au kupotea,
bandia vya mawasiliano katika soko.chanzo jami forums.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top