Breaking News
Loading...

Advert

Saturday, January 28, 2017

Soma simulizi ya ERIC SHIGONGO.DIMBWI LA DAMU-13.soma zaid

ERIC SHIGONGO
DIMBWI LA DAMU-13
Baada ya Manjit kukabidhiwa �kampuni yake na
Multilat�eral Investiment Inc. kwa haraka
alichukua uamuzi wa kuibadilisha kampuni yake
jina na kuiita Canada Oils & Gas Inc. Mabadiliko
hayo yaliwafanya watu wengi kuamini Manjit
angeweza kuiendesha vizuri kampuni yake.
Alipangua ngazi zote za uongozi kuanzia juu hadi
chini na aliajiri Mkurugenzi mpya aliyemtoa katika
kampuni ya Multilateral. Yeye alibaki kama
mwenyekiti wa kampuni hiyo, mama yake pamoja
na Victoria wakawa wajumbe wa bodi.
Miaka mitatu iliyofuata kampuni yake ilishuhudia
mafanikio makubwa kupita kiasi, vituo vya mafuta
viliongezeka katika nchi nzima ya Canada!
Canada oil & Gas Inc ilimiliki vituo vitatu hadi
vinne vya mafuta katika kila miji mikuu yote
nchini humo. Manjit akabadilika na mtu
mashuhuri na kijana tajiri kuliko hata alivyokuwa
baba yake.
“ Mama! Nitajitahidi kufanya kazi kwa nguvu zote
ili tufanikiwe zaidi!”
“Sawa mwanangu, kila utakachofanya ni sawa
kwangu!”
Maneno ya mama yake yalimpa moyo sana
Manjit, mwaka huo huo ilitangazwa tenda ya
kuliuzia mafuta Dizeli na Petroli jeshi la nchi hiyo,
ilikuwa ni tenda ya mamilioni ya dola za
kimarekani na ilikuwa ni kazi kubwa kuliko kazi
zote alizowahi kufanya tangu akabidhiwe
kampuni.Wafanyabiashara wengi nchini Canada
waliitaka kazi hiyo na kampuni ya Canada Oils&
Gas nayo ilikuwa miongoni mwa kampuni
zilizoiomba.
“Mama ni lazima tufanye lolote linalowezekana
kuhakikisha tunapata tenda hii?”
“Fanya lolote mwanangu, kila kitu ni ruksa!”
“Ni lazima tutumie pesa mama! Sababu
wanasema tumia pesa ili upate pesa!”
“Sawa tu mwanangu!”
Hilo ndilo alilofanya Manjit, alitumia pesa nyingi
kuwahonga watu wote waliokuwa na mamlaka ya
kuitoa tenda mpaka akaibuka mshindi! Ilikuwa ni
furaha kubwa mno kwa Manjit, mama yake,
Victoria na hata wafanyakazi wengine wa
kampuni hiyo! Walijua kupatikana kwa kazi hiyo
kungeongeza maslahi yao.
“Mama tumetajirika!”
“Hakika mwanangu! Nimeamini una akili”
“Itabidi nisafiri hadi Iran kwenda kuongea
biashara na matajiri wa huko ikiwezekana tuwe
tunapata mafuta ya mkopo kutoka kwao na
kuwalipa baada ya kupata malipo yetu kutoka
serikalini!”
“Fanya uwezalo!”
Wiki moja baada ya kupata tenda hiyo ilibidi
Manjit alisafiri hadi Iran ambako aliongea na
wafanyabiashara wengi wenye visima vya mafuta
lakini hakufanikiwa kupata hata mmoja aliyekuwa
tayari kufanya naye biashara, kila aliyemfuata na
kumweleza kuwa mahitaji yake ya mafuta
yalikuwa mapipa milioni mbili kwa mwezi, aliiona
kazi hiyo ni kubwa sana na kukiri asingeweza
kukidhi haja yake!
“Nafikiri ungejaribu Iraq kuna kampuni moja
inaitwa Gulf Gas Limited hiyo inaweza kukupa
mafuta hata zaidi ya hayo!”
“Inamilikiwa na nani?”
“Awali ilimilikiwa na Mohamed Mashreef huyo
alikuwa mfanyabiashara wa Kiarabu lakini
alifariki na kumrithisha Mwafrika mmoja,
ninavyosikia yeye pia ni mgonjwa kazi zote hivi
sasa zinaendeshwa na mtoto wake aitwaye
Patrick!”
“Patrick?”
“Ndiyo!”
“Mbona jina si la kiarabu?”
“Ni mchanganyiko wa Mwarabu na Mtanzania!”
“Mtanzania?”
“Ndiyo, baba yake alitokea Tanzania miaka mingi
iliyopita!”
“Nahitaji kumwona!”
“Basi safiri mpaka Iraq!”
Siku hiyo hiyo jioni Manjit alipanda ndege na
kusafiri hadi Baghadad ambako aliingia usiku na
kushindwa kumtafuta tajiri Patrick ikabidi alale
mpaka siku iliyofuata asubuhi alipokwenda ofisini
kwake! Nje ya ofisi hiyo kulikuwa na idadi kubwa
sana ya maaskari walionekana kuimarisha ulinzi
lakini Manjit alifanikiwa kuingia hadi mapokezi
baada ya kujitambulisha, mapokezi alipokelewa
na msichana mrembo wa Kiarabu na
kukaribishwa aketi kitini!
“Can I see the Director?”
“Sorry the Director is not around! He is admitted
in hospital, but his Deputy is around, would you
like to see him?” (Mkurugenzi hayupo lakini Naibu
wake yupo, je ungependa kumwona yeye?)
“Yeah! Because this is an official matter I think it
can be be handled by any authority! (Ndiyo kwa
sababu hili ni suala la kikazi na linaweza
kushughulikiwa na mtu yeyote!)
Baada ya jibu hilo msichana huyo alinyanyua
simu yake na kubonyeza namba fulani kisha
akaanza kuongea na mtu wa upande wa pili na
kumueleza kuwa palikuwa na mgeni aliyetaka
kumuona! Alipoweka simu yake chini alimuashiria
Manjit aingie ndani! Alinyanyuka na kuanza
kutembea taratibu akiufuata mlango uliokuwa
kulia kwake ilikuwa ni ofisi ya kifahari,
iliyopambwa na vioo kila upande! Iliashiria kuwa
mwenye ofisi hiyo alikuwa na uwezo mkubwa
kipesa! Manjit aliingia ndani akiwa na hamu
kubwa ya kumuona Patrick, mawazoni kwake
alifikiri mtu huyo alikuwa anakwenda kumwona ni
mnene na mzee lakini alishangaa kukuta mtu
aliyekuwa akimtafuta ni kijana mdogo kuliko hata
yeye!
“You are welcome sir!”(Karibu sana bwana!)
“Thank you! I’m Mr. Manjit Shabir!”(Ahsante!
Ninaitwa Bwana Manjit Shabir)
“Manjit Shabir? The owner of the Oil company in
Canada!”(Manjit Shabir? Mwenye kampuni ya
Mafuta Canada?)
“Oh yeah!How did you recognise me?”(Ndiyo
umenigunduaje?)
“Nice to meet you Sir, I’m Patrick N. Abdulwakil I
have been hearing of your name so many times
and really wanted to meet you one day! Today
my dream has come true!”(Nimefurahi kukutana
na wewe! Ninaitwa Patrick N. Abdulwakil
nimekuwa nikisikia jina lako mara nyingi na
nilitaka sana kukutana na wewe siku moja! Leo
ndoto yangu imetimia!) Alisema Patrick
akinyanyuka na kumkumbatia Manjit, walionyesha
furaha kubwa sana.
Waliongea mambo mengi kuhusu biashara yao ya
mafuta na hatimaye kufikia muafaka wa kufanya
biashara kwa ushirikiano! Patrick alikubali
kumuuzia Manjit mafuta kwa mkopo kwake kazi
yake pekee ingekuwa ni kuyasafirisha mafuta
kutoka Baghdad kwenda Montreal Canada na
angetakiwa kulipa pesa baada ya kuyauza
mafuta kwa jeshi! Kwa Manjit mambo yalikuwa
kama alivyopanga, hakutegemea mipango
ingekuwa rahisi kiasi kile furaha yake ilizidi
kuongezeka.
“Lakini kumbuka kuwa kampuni yangu
haitawajibika na hasara yoyote itakayotokea
katika usafirishaji wa mafuta, hata kama meli
itazama sisi tutakachojua ni kulipwa pesa yetu
tu, sijui jambo hilo utaliweza?”
“Haina shida kabisa Patrick! Hilo litafanyika!”
Alijibu Manjit na mkataba ulisainiwa siku hiyo
hiyo Manjit aliondoka kurudi Canada bila kuelewa
undugu na uhusiano uliokuwepo kati yao.
***************
Kwa Manjit kupata tenda ya kuliuzia jeshi mafuta
ilikuwa furaha kubwa na dalili ya mafanikio lakini
kwa wafanyabiashara wenzake walioikosa tenda
hiyo hasira ziliwajaa, hasira zilizojaa chuki dhidi
ya Manjit hasa baada ya kugundua kuwa Manjit
alitumia pesa kuwahonga viongozi wa jeshi ndio
akapata tenda hiyo, walichukia mno na
kulazimika kuunda umoja wa kupambana naye,
waliahidi kumkwamisha katika biashara zake
zote!
“Ni lazima aanze moja, naona hizi mali za kurithi
zimempa kiburi anashindwa kuheshimu wazee,
huyu ni mtoto mdogo sana hawezi kutusumbua
sisi!” Alisema bwana Davids, mmiliki wa kampuni
ya kusafisha mafuta machafu nchini Canada,
Crude Oils Inc.
“Kweli! Ni lazima tumkomeshe” Wenzake watano
waliitikia.
Mipango mingi ilipangwa usiku huo ili
kumwangusha Manjit kibiashara, matajiri
waliokosa tenda ya kuuza mafuta jeshini
waliunganish nguvu zao ili kupambana nae!
Miongoni mwa mipango yaliyopanga ni kumuua
Manjit mwenyewe na kama si yeye basi mama
yake au Victoria! Ili mradi tu kuhakikisha anarudi
nyuma na kufilisika kabisa! Hawakuwa tayari
hata kidogo kuona mtoto mdogo tena mgeni
katika nchi yao akitajirika mbele ya macho yao!
“Nitazilipua meli zote za mafuta zitakazokuwa
zikibeba mafuta yake kutoka Iraq kuja hapa
Canada! Hilo niachieni mimi” Alisema Alexandria
mmiliki wa vituo vya mafuta vya CanadOils
“Nitatuma watu kuivamia nyumba yake na kila
mtu atakayekuwemo ndani siku hiyo ni lazima
afe hata yeye mwenyewe!” mfanyabiashara
mwingine aliahidi.
“Nitatumia watu wa Mamlaka ya kodi ili
wayakague mahesabu yake kuona kama analipa
kodi, nina uhakika atakuwa na matatizo
makubwa! Na hapo ndipo tutakapomaliza!
Canadian Revenue Authority watakamata mali
zake zote!” Mwingine tena aliongea kwa hasira!
Yote yaliyosemwa katika mkutano huo hayakua
utani, wazee hao walidhamiria kumkomesha
Manjit! Walidhamiria kumfanya masikini na hata
kumuua kabisa yeye na familia yake yote. Manjit
hakujua lolote lililoendelea mioyoni mwa
wafanyabiashara wenzake na aliamini hakuna
aliyeijua siri yake ya kushinda zabuni hiyo ya
kuuza mafuta.
********************
Meli tatu za kwanza zilizobeba matenki ya
mafuta ya karibu dola milioni 120 ambazo kwa
wakati huo zilikuwa sawa na shilingi za
Kitanzania Bilioni 84 zilikuwa zikisafiri katika
bahari ya Hindi kuelekea Canada, pamoja na
kubeba mafuta ndani ya meli hizo kulikuwa na
wafanyakazi wasiopungua mia mbili na kumi!
Huo ndio ulikuwa mzigo wa kwanza ambao
Manjit alitegemea kuumwaga jeshini Canada na
kupata faida ya dola za Kimarekani zisizopungua
200! Ilikuwa ni faida kubwa mno iliyompa uhakika
asilimia mia moja kuwa kama angefanya
biashara hiyo kwa mwaka mmoja angeweza
kutajirika pengine kuliko mtu mwingine yeyote
katika nchi hiyo.
Alikuwa nyumbani kwake akipumzika na familia
yake ikiwa ni siku mbili tu tangu aongee na tajiri
Patrick akipewa taarifa kuwa tayari mzigo
ulishaondoka nchini Iraq na ulitegemewa kuingia
Canada baada ya wiki tatu! Ghafla simu yake
iliita na mama yake aliipokea na kumpa Manjit.
“Hallow! Manjit anaongea nani mwenzangu?”
“Mimi ni Patrick!”
“Ndiyo za tangu juzi?”
“Ni nzuri lakini sio nzuri sana!”
“Unaumwa?”
“Hapana ila nina taarifa mbaya kidogo, meli zote
zilizoondoka hapa na mafuta zimelipuliwa!
Wafanyakazi wote wamekufa na meli bado
zinawaka moto huku matuta yakimwagika
baharini, nilipoteza nao mawasiliano tangu jana
leo nimepokea simu ya upepo kutoka kwenye
meli ya Atlantic Sailors, wamenitaarifu kuwa
waliiona meli yetu ikiwaka moto baharini! ”
“Mungu wangu unaniambia kweli?”
“Huo ni ukweli siwezi kukudanganya hata mimi
nimechanganyikiwa! Nafikiri kwako itakuwa
hasara kubwa sana, kwa kweli biashara
umeianza vibaya kwani sisi mafuta yetu itabidi
yalipwe kama kawaida!”
Taarifa hiyo ilimfanya Manjit alie machozi kwani
zilikuwa ni habari mbaya mno kwake, alijua ni
njama lakini alishindwa kuelewa ni nani
aliyezifanya hata mama yake pamoja na Victoria
nao walishindwa kuvumilia wakajikuta
wakibubujikwa na machozi!
Siku iliyofuata ilibidi Manjit asafiri hadi Iraq
kuongea na Patrick ambaye aliendelea kusisitiza
juu ya makubaliano yao katika mkataba ulioeleza
wazi kuwa Manjit alitakiwa kulipa pesa zote
alizodaiwa pamoja na kuwa mafuta yalimwagika
baharini! Manjit hakuwa na ubishi alikubali
kufanya hivyo lakini si kwa wakati huo.
Patrick alikubali na kumpakilia tena meli nyingine
nne zenye mafuta ya thamani ya dola milioni 600
ambazo kwa shilingi za Kitanzania zilikuwa ni
sawa na bilioni 480 kwa wakati huo, lakini pia
meli hizo hazikufanikiwa kufika nchini Canada,
zikiwa katika eneo lile lile zilipolipukia meli za
mwanzo nazo ziliangushiwa mabomu na kulipuka!
Mafuta yote yalimwagika na watu wote
waliokuwemo waliteketea kwa moto, Manjit alizidi
kuchanganyikiwa na kushindwa kuelewa ni nani
aliyekuwa akimfanyia ukatili huo!
Alipoongea na Patrick juu ya tatizo hilo yeye
aliendela kusisitiza juu ya malipo yake! Tayari
deni lilishafika dola za Kimarekani milioni 720
Zilikuwa ni pesa nyingi mno kwake kuzilipa na
kuendelea kufanya biashara, pamoja na matatizo
yote hayo Manjit hakukata tamaa alijipa
matumaini kuwa angeweza kulipa deni hilo baada
ya kufanya biashara na jeshi kwa muda, hivyo
aliomba apakiliwe mafuta mengine tena na
Patrick alikubali.
Kwa hasira ya kufidia safari hii alipakia katika
meli saba zote zikiwa na mafuta ya thamani dola
milioni 800, ilikuwachenga waliokuwa
wakimhujumu nne kati ya meli hizo zikapita njia
ya kawaida na tatu zikapitishwa njia ya
mzunguko wa CapeTown, Afrika Kusini kisha
kwenda Afrika ya Magharibi na baadaye kuingia
Canada, kwa njia hiyo Manjit aliamini angeweza
kufikisha mafuta yake hata kidogo.
Meli zote saba hazikufanikiwa kufika Canada,
zote zililipuliwa zikiwa njiani! Manjit
alichanganyikiwa zaidi, deni alilokuwa nalo kwa
Patrick lilimtisha! Aliamini tayari alishakuwa
masikini na angeweza hata kufungwa gerezani
kama angeshindwa kulipa pesa za Patrick.
Kwa hakika maadui zake tayari walishafanikiwa
kumporomosha. Akilia machozi aliamua kurudi
nyumbani kutafuta pesa za kumlipa Patrick.
*******************
Aliteremka uwanja wa ndege wa Ottawa saa
kumi na mbili jioni na kuchukua teksi.
“Nipeleke Carvin Avenue!”
“Sawa mzee!”
Gari liliondoka uwanja wa ndege kwa kasi na
kadri lilivyozidi kuyakaribia maeneo ya nyumbani
kwake Manjit alizidi kusikia kelele za ving’ora vya
magari ya zimamoto! Awali alifikiri yalikuwa ni
mambo ya kawaida katika jiji hilo lenye watu na
pilikapilika nyingi za maisha, lakini hatua chache
kabla ya kufika nyumbani kwake alishangaa
kuona moshi mkubwa angani, alipoingalia nyumba
yake hakuiona ilikuwa katikati ya moshi. Moto
mkubwa ulikuwa ukiiteketeza, zimamoto
walikuwa wakijitahidi kuzima lakini walishindwa.
Hakufikiria kitu kingine chochote, mawazo yake
yalimpeleka kwa mama yake mzazi pamoja na
Victoria aliowaacha ndani ya nyumba yake! Kwa
haraka aliruka garini na kuanza kukimbia mbio
kuelekea kwenye moto huo mkubwa huku akiliita
jina la mama yake! Aliona ni heri kufa kuliko
kupambana na matatizo yaliyokuwa yakimfuata,
mbele kidogo alisita na kusimama, woga wa
kuungua na moto ulimwingia.
Kwa hakika dunia ilikuwa imemgeuka! Deni la
mafuta alilokuwa akidaiwa hakuwa na uwezo wa
kulilipa na bado nyumba yake ilikuwa ikiwaka
moto na hakuwa na uhakika kama mama yake
pamoja na Victoria walikuwa hai au walikuwa
wakiteketea ndani ya moto huo.
Kwa jinsi umati mkubwa wa watu ulivyokusanyika
hakuna mtu aliyegundua kuwa Manjit alikuwepo
eneo la tukio, akiwa amesimama wima huku
akitetemeka alisikia sauti ya mama yake ikiliita
jina lake kutoka katikati ya moshi mkubwa
uliotanda eneo hilo, hiyo ilimaanisha mama yake
alikuwa bado amekwama ndani ya nyumba
iliyokuwa ikiwaka moto!
Moyo wake ulimuuma kupita kiasi na kujikuta
akipata ushujaa wa ajabu na kuanza kukimbia
mbio kuelekea ndani ya nyumba iliyokuwa
ikiwaka moto bila woga kama ilivyokuwa awali.
Manjit alijua yaliyotokea yote yalikuwa ni hujuma
lakini hakujua ni nani aliyemfanyia hujuma hiyo
mbaya.
Watu waliokuwa eneo hilo walimwona mtu
akikimbia kuingia ndani ya moto, kitendo hicho
kiliwashangaza sana na kujikuta wakijaribu
kukimbia kwa nyuma wakimfuata kwa lengo la
kumuokoa lakini tayari Manjit alishapotelea ndani
ya moshi mkubwa uliokuwa umetanda! Walijua
naye anakwenda kuteketea.
“Huyu sijui mjinga? Sasa kwanini ameingia ndani
ya nyumba inayowaka moto kiasi hiki?” Walijiuliza
baada ya kushindwa kumpata.
Je, nini kitaendelea?
Tukutane wiki ijayo hapahapa.
Unaweza kuendelea kuifuatilia kwa kuLIke.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top