Breaking News
Loading...

Advert

Friday, January 27, 2017

Inadanaiwa wanajeshi wanahusika kwenye mau.aji ya kondakta wa daladal mkoani Tanga.soma zaid

AzamTV News imeripoti kwamba Inadaiwa
Wanajeshi wamehusika kwenye mauaji ya kijana
mmoja wa Tanga ambaye kazi yake ilikua ni
Kondakta wa daladala.
Mmoja wa Wananchi waliohojiwa na AzamTV
amesema kilichotokea ni Mwanafunzi wa kike
ambaye ni mtoto wa Mwanajeshi kupanda
Daladala bila kulipa nauli lakini Kondakta
akachukua maamuzi ya kumzuia yule binti
kwamba lazima alipe nauli.
Inadaiwa Baba mzazi wa Binti huyo ambaye ni
Mwanajeshi aliagiza vijana kwenda kumkamata
Kondakta na kumpeleka kwenye kambi ya Jeshi
na wakampiga mpaka hali yake ikawa mbaya
kisha wakamrudisha nyumbani kwake na baadae
watu wakaona akichukuliwa na kupelekwa
Hospitali akiwa ameshafariki.
Sehemu ya Wananchi wengine waliotoa maoni
yao ni Mwanamke mkazi wa Nguvumali aliesema
huyu ni mtu wa tatu anauwawa na Wanajeshi
kwenye mji wa Tanga ‘ Wamezidi kutuonea ndio
kawaida yao… tumechoka’
Kamanda wa Polisi Tanga Benedict Wakulyamba
amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema
mpaka sasa watu watatu wanashikiliwa na Polisi
na taratibu za upelelezi zikikamilika hatua dhidi
yao za kufikishwa Mahakamani zitachukuliwa.
‘ Tukio kufanyikia kwenye kambi ya jeshi haina
maana kwamba Wanajeshi wamehusika
kwasababu ndani ya kambi ya jeshi tunazo
familia za Askari ambao sio Askari bali ni raia
wa kawaida na ndio maana mpaka sasa
tunaowashikilia kuanzia yule binti ni raia tu wa
kawaida pamoja na hao wengine tuliowakamata‘
– Kamanda Wakulyamba

0 comments :

Post a Comment

Back To Top