Breaking News
Loading...

Advert

Tuesday, May 10, 2016

Kampuni sita za maji kenya zafungwa.soma zaid.


Shirika la kukadiria ubora wa bidhaa nchini
Kenya KEBS limefunga viwanda sita vya kupakia
maji ya chupa kwenye kampeni inayoendelea ya
kudhibiti maji machafu ya kunywa.
Aidha serikali ya kaunti ya Mombasa pia imepiga
marufuku uuzaji wa baadhi ya maji chupa baada
ya kuzipata na maradhi.
Zaidi ya kampuni mia sita nchini Kenya zina
leseni ya kupakia maji ya chupa, lakini kuna hofu
kwamba kampuni bandia ni zaidi ya hiyo.
Maji ya chupa huuzwa sana kwenye maduka ya
bara Afrika, lakini nchini Kenya si yote ni masafi.
Shirika la kukadiri ubora linaonya wateja kwamba
maji ya chupa wanayokunywa si masafi kama
yanavyouzwa.
Jijini Mombasa pekee, kampuni sita zimefungwa
kwa kupakia maji machafu.
Aidha idara ya afya Mombasa imepiga marufuku
uuzaji wa baadhi ya maji yanayouzwa baada ya
chembe za bacteria zinazopatikana kwenye
kinyesi kupatikana kwenye maji hayo.
Mombasa imekabiliwa na kuenea kwa ugonjwa
wa Hepatitis A, ambao husambazwa kwa virusi
Zaidi kutokana na kwa kunywa maji au kula
chakula kilicho na virusi hivyo.
Wakazi wengi kwenye miji ya Kenya hawaamini
kunywa maji ya mifereji baadhi ya wataalamu
wengine huonya kwamba maji ya mifereji
huchanganyika na maji taka kwenye mabomba.
Shirika sasa linapania kuboresha alama yake ya
viwango, ili kutenga bidhaa duni kutoka sehemu
za mauzo.chanzo bbc swahil

0 comments :

Post a Comment

Back To Top