Kwa mara ya kwanza rais obama ameweka historia.soma zaid.
Rais wa Marekani Barrack Obama anatarajiwa
kutembelea Hiroshima mwezi huu akiwa ni rais
wa kwanza aliyepo madarakani kufanya ziara ya
mji huo wa Japan tangu ushambuliwe na bomu
la kinyuklia la Marekani 1945.
Ziara hiyo itakuwa miongoni mwa ziara za bara
Asia kuanzia tarehe 21-28 mwezi Mei ambayo
pia itashirikisha Vietnam.
Bomu la Hiroshima mnamo tarehe 6 gosti mwaka
1945 liliwaua watu 140,000.
Pamoja na bomu la pili katika mji wa Nagasaki
linasifika kwa kumaliza vita vya dunia vya pili.
Jimmy Carter amezuru Hiroshima lakini baada ya
kukamilika kwa utawala wake.
Taarifa kutoka kwa Obama imesema kuwa rais
atafanya ziara ya kihistoria huko Hiroshima na
waziri mkuu Shinzo Abe ili kuangazia kuhusu
ushirikiano uliopo wa kuleta amani na usalama
katika dunia iliojaa zana za kinyuklia.chanzo bbc swahil
0 comments :
Post a Comment