Breaking News
Loading...

Advert

Tuesday, May 10, 2016

Tamasha la beyonce lavamiwa na maandamano ya polisi huko houston.soma zaid.


Kundi moja la maafisa wa polisi limefanya
maandamano karibu na tamasha lililofanyika
katika mji wa nyumbani wa nyota wa muziki
Beyonce huko Houston.
Wanachama wa muungano wa polisi na Sherrif
walisimama mbali na uwanja wa soka na
kuelekeza mwangaza wa bluu katika ukumbi wa
tamasha hilo.
Walikuwa wanapinga kanda ya video ya Beyonce
ambayo wanasema inawaponza polisi.
Mwanamuziki huyo tayari amesema kwamba
hawakosoi polisi katika wimbo huo na kusema
kuwa maafisa wa polisi wanaodhani aliwaponza
wanakosea.
Mwanachama mmoja wa polisi amekiambia
chombo cha habari KHOU11 kwamba
hawakufurahia baada ya Beyonce kutumia picha
za gari moja la polisi mjini New Orleans iliokuwa
ikizama katikamafuriko.
''Tunaamini kwamba baadhi ya mambo yake ni
kinyume na maafisa wa polisi'',alisema.
Mnamo mwezi Aprili,Beyonce aliambia jarida la
Elle kwamba anaheshimu polisi lakini hapendi
unyanyasaji.
''Mtu yoyote anyedhani kwamba siwapendi polisi
anakosa kwa sababu'', alisema.
''Ninawapenda na kuwaheshimu sana polisi
pamoja na familia za maafisa hao ambao
hujitolea ili kuhakikisha tuko salama''.chanzo bbc swahil

0 comments :

Post a Comment

Back To Top