Katika kutatua tatizo la sukari serikal imeagiza tani70,000 za sukari nje.soma zaid
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amesema Serikali imeagiza kutoka nje
ya nchi tani 70,000 za sukari ambapo
kati ya hizo, tani 11,957 zimeshawasili
nchini na zitaanza kusambazwa kesho
(Jumatano).
Ametoa kauli hiyo leo mchana
(Jumanne, Mei 10, 2016) wakati
akizungumza na waandishi wa habari
kwenye mkutano uliofanyika nyumbani
kwake Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Akitoa ufafanuzi wa sukari ambayo
imekwishawasili nchini, Waziri Mkuu
alisema tani 2,000 zitapelekwa mikoa
ya Kaskazini, tani 3,000 (mikoa ya
Kanda ya Ziwa), tani 2,000 (mikoa ya
Kusini), tani 2,000 (Nyanda za Juu
Kusini) na tani 2,000 (mikoa ya Kanda
ya Kati).
“Tani nyingine 24,000 za sukari
zitawasili Ijumaa hii na hadi zitoke
bandarini itakuwa kama Jumapili kwa
hiyo zinaweza kusambazwa kuanzia
Jumatatu. Tani nyingine 20,000
zitawasili baadaye, ama mwishoni mwa
mwezi huu au mapema mwezi Juni,”
alisema Waziri Mkuu.
Amesema anawataka Watanzania
wasihofu kuhusu uhaba wa sukari
uliojitokeza hivi karibuni kwani
umesababishwa na watu wachache.
“Mheshimiwa Rais ameagiza watu
waliohodhi bidhaa hii wakamatwe na
sukari isambazwe. Lakini pia tunaagiza
kwa muda mfupi kwa sababu viwanda
vyetu vinatarajia kuanza uzalishaji
ifikapo Julai,” alisema.
Amewataka wasambazaji wa sukari
waziuze kwa wafanyabishara wadogo
ili wao wawawuzie wananchi kwa bei
elekezi ya sh. 1,800. Pia amewaagiza
Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya
kuhakikisha wanasimamia zoezi la
ukaguzi ili kubaini zaidi wale
waliohodhi bidhaa hiyo.
Akifafanua kuhusu mkakati wa Serikali
kuongeza uzalishaji wa sukari nchini,
Waziri Mkuu amesema nia ya Serikali
ni kuhakikisha tatizo la uhaba wa
sukari nchini linakwisha ifikapo 2019.
“Wananchi wasiogope, Serikali
imechukua hatua kwa udhibiti mzuri ili
tusije kuporomosha soko letu la
ndani,” alisema.
“Tunao mkakati wa kuboresha viwanda
vya ndani, wenye viwanda wenyewe au
kwa ubia na wawekezaji kutoka nje,
wanaweza kufungua mashamba
kwenye maeneo matatu tuliyotenga
kwa ajili hiyo,” alisema.
“Serikali imetenga maeneo matatu
yanayofaa kwa kilimo cha miwa huko
Bagamoyo, Ngerengere na Kigoma.
Huko wanaweza kulima na kujenga
viwanda vya sukari na uzalishaji
ukawa unapanda mwaka kwa mwaka
hadi tutakapoweza kuimaliza hii gap
iliyopo,” alisema.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMANNE, MEI 10, 2016.
0 comments :
Post a Comment