Breaking News
Loading...

Advert

Thursday, May 12, 2016

Wazir mkuu wa uingereza kutangaza haya kuhusu ufisadi.soma zaid.

Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron
anatarajiwa kutangaza katika mkutano wa
kupinga ufisadi kwamba makampuni ya ng'ambo
yanayomiliki mali London yatalazimishwa
kujisajili wazi wamilki mali hiyo.
Hatua hiyo imeundwa imeidhinishwa kuzuia
wafisadi na nchi dhidi ya kuhamisha, na kuficha
fedha kupitia soko la London. Nchi kadhaa
nyengine huenda pia zikaahidi kuidhinihsa usajili
wa wamilki asili wa makampuni.
Kuna takriban kampuni 100,000 England pamoja
na Wales zinazomilikiwa na makampuni ya nje
nyingi zikiwa mjini London.
Zina thamani ya mamilioni ya pauni na nyingi
hutumiwa kuficha fedha ambazo zimepatikana
kwa njia za kifisadi.
Katika siku zijazo kampuni yoyote itakayo taka
kununua au kumiliki mali ni lazima ijisajili.
Baadhi ya maenoe ya Ukngereza na milki zake
zitajiunga nchi nyingine 33 katika kukubali
kudhirisha usajili wa wamilki kampuni, taarifa
zinazopaswa kuwa wazi kwa polisi .
Kutakuwa na kituo cha ushirikiano cha
kukabiliana na ufisadi London na hatua kubwa
zitachukuliwa dhidi ya wakuu wanaoshindwa
kuzuia udanganyifu au ulanguzi wa fedha katika
kampuni zao.
Mtihani wa mpango wa waziri mkuu Cameron
utakuwa ni nchi ngapi nyingine zitakazofuata
mfano huo.
Kwa mfano Virgin Islands haihudhirii mkutano
huo na haijakubali kutoa taarifa zozote kuhusu
kampuni zilizoko huko.chanzo bbc

0 comments :

Post a Comment

Back To Top