Breaking News
Loading...

Advert

Thursday, June 16, 2016

Mbuzi wa ajabu watikisa Dar.soma zaid.


DAR ES SALAAM: Dunia ina mambo! Mbuzi
wanaosemwa kuwa ni wa ajabu, wanatikisa Jiji
la Dar es Salaam, baada ya kuonekana katika
maeneo mbalimbali wakijichunga bila mwenyewe
kufahamika, lakini wakiwa hawaibiwi wala
kubughudhiwa, Risasi Mchanganyiko lina
mkanda wa kusisimua.
Mbuzi hao wamekuwa wakijiongoza wenyewe,
wakila majani hadi kwenye matuta ya barabara
zilizopo katika maeneo mbalimbali ya jiji, jambo
linalosababisha minong’ono na simulizi kadhaa
kwa watu. Jambo lingine linalowahusu mbuzi hao
ni ukweli kuwa licha ya kuonekana wako peke
yao usiku na mchana, lakini hakuna mtu yeyote
anayewaiba, licha ya jiji hilo kuwa na idadi kubwa
ya vibaka na wezi pengine kuliko mikoa yote
nchini.
Simulizi zinadai, mtu yeyote anayethubutu kuwaiba
au kuwadhuru kwa namna yoyote, hupatwa na
madhara, jambo linalowafanya kuogopewa. Baadhi
ya maeneo ambayo wanyama hao
wameshuhudiwa na gazeti hili wakijichunga bila
kuongozwa ni Ubungo, Mbezi Beach, Tegeta na
maeneo ya Viwanja vya Leaders vilivyoko
Kinondoni. Risasi Mchanganyiko lilifanikiwa
kuzungumza na baadhi ya wananchi wa maeneo
tajwa kuhusu mbuzi hao.
“Mimi nilishuhudia watu wakiwapakia mbuzi hawa
usiku mwingi, nilijua kwa vyovyote hao ni wezi
maana mwenyewe hawezi kuja kuwachukua
usiku, lakini sikujishughulisha nao kwa sababu
hata mmiliki halali simjui. Lakini asubuhi yake
nilipopita nikawakuta, nikapata hamu ya kujua
kulikoni.
“Nilipoulizia, nikaambiwa eti wezi wale
walikwenda nao huko Kisarawe mkoani Pwani,
lakini walipotaka kuwashusha wakagoma,
walitumia kila njia wakashindwa, wakaogopa na
wakaamua kuwarudisha, cha ajabu walipofika
eneo lao tu, kabla hata hawajashushwa walianza
kuruka wenyewe kutoka kwenye gari,” alisema
Emmanuel Juma wa Tegeta.
Naye Zuwena Hamis mkazi wa Ubungo alisema
mbuzi hao wameshazoeleka, kwani wakati
mwingine hutanda barabarani kiasi cha kuyazuia
magari maana mtu akiwagonga tu, lazima apate
ajali. “Ole wako umpige, utakiona cha moto, juzi
walilala barabarani magari yakashindwa kupita na
kufanya madereva wageuze kwani wanaho_ a
ukimgonga mmojawapo hau_ ki Mkuranga,”
alisema.
Gazeti hili lilimtafuta Msemaji wa Halmashauri ya
Jiji la Dar es Salaam, Gaston Mwakyembe ili
azungumzie hatua zinazochukuliwa na jiji katika
kuwadhibiti mbuzi hao kutokana na uchafuzi wa
mazingira, lakini simu yake ilirudisha ujumbe wa
kuomba udhuru, akiahidi kupiga muda mfupi ujao.
Hata hivyo, alipotafutwa tena baada ya saa mbili,
simu hiyo haikupatikana kabisa.chanzo amani

0 comments :

Post a Comment

Back To Top