Mwanamke mmoja atiwa mbaroni kwa kutupa mapacha 2 mkoani Arusha.soma zaid.
ARUSHA: AMENASWA! Msako uliofanywa na
wananchi wa Kitongoji cha Namayana, Kata ya
Kiranyi wilayani Arumeru mkoani hapa, kufuatia
tukio la mwanamke kudaiwa kutupa vichanga
mapacha, umefanikiwa kumnasa mtuhumiwa
Happiness Joel (29), tembea na Amani.
Mwenyekiti wa kalisema June 7, mwaka huu alipata taarifa ya
kutupwa kwa vichanga viwili katika chemba ya
choo kinachomilikiwa na mkazi wa kitongoji
hicho, Elibariki Loti.
Alisema baada ya taarifa hiyo, yeye na wananchi
walikwenda kushuhudia na kukuta vichanga hao
wamefariki dunia na kutoa taarifa kwa jeshi la
polisi huku yeye na wananchi wake wakianzisha
msako mkali kumbaini mwanamke aliyekuwa na
ujauzito.
“Polisi walifika na kuchukua miili ya vichanga
hao na kwenda kuihifadhi katika chumba cha
maiti katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru
kusubiri uchunguzi,” alisema mwenyekiti huyo.
Akipandishwa kwenye gari la polisi.
Aliendelea kuweka wazi kuwa June 8, mwezi huu,
yaani siku moja baada ya tukio hilo, wananchi
walifanikiwa kumbaini mtuhumiwa huyo ambaye
pia alikuwa na mtoto wa miaka 2 mgongoni na
baada ya kuhojiwa, alikiri kuhusika na tukio hilo.
Alisema mtuhumiwa huyo alieleza kwamba ni
kweli alikuwa na ujauzito na aliamua kutupa
vichanga hivyo baada ya kujifungua kwa kile
alichodai ni bahati mbaya.
Hata hivyo, taarifa nyingine zinadai kuwa mama
huyo aliwatupa watoto hao kutokana na aibu
baada ya kuwa tayari ana mtoto mdogo
mgongoni ambaye bado anamnyonyesha.
Kwa upande wa mwanaume aliyempa ujauzito
huo aliyetambulika kwa jina moja la Godlucky,
alikiri kumpa ujauzito mwanamke huyo na
kusema kuwa amesikitishwa na tukio hill.
0 comments :
Post a Comment