Kocha wa yanga ameiomba CUF kuchukua hatua.soma zaid.
KOCHA Mkuu wa Yanga Hans Pluijm ameliomba
Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) kuchukua
hatua kali kwa klabu ambayo mashabiki wake
wataleta vurugu kwa timu pinzani kwenye hatua
ya makundi ya michuano ya Kombe la Shirikisho
la Soka Afrika (CAF CC).
Yanga itakuwa mgeni wa klabu ya Mo Bejaia
kwenye mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi
ya mashindano ya CAFCC mwishoni mwa wiki hii
nchini Algeria.
Pluijm mwenye uzoefu wa mashindano makubwa
Afrika, alisema katika mahojiano maalumu na
gazeti hili kwa njia ya mtandao kuwa kwa miaka
mingi kumekuwa na vitendo vya vurugu kwenye
soka la Afrika, ambapo timu mwenyeji imekuwa
ikiifanyia timu ngeni.
Alitolea mfano wa vurugu ambazo Yanga
walifanyiwa kwenye mchezo wa Ligi ya
Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri
ugenini na dhidi ya Sagrada Espranca nchini
Angola na kusema vitendo hivyo havina budi
kukomeshwa.
“Vitendo vya vurugu dhidi ya timu ngeni katika
soka la Afrika sio vya sasa, vipo kwa miaka
mingi sana. Sisemi natarajia kukutana navyo
katika mchezo dhidi ya Mo Bejaia au la, lakini
tunatakiwa kujiandaa kisaikolojia kwa lolote.
“CAF wanapaswa kuwa wakali dhidi ya vitendo
hivi vya vurugu vinavyofanywa na timu wenyeji
kwa wageni wao. Wanatakiwa kuchukua hatua
kali,” alisema Pluijm ambaye yuko na timu yake
nchini Uturuki ikijiandaa na mchezo huo.
0 comments :
Post a Comment