Breaking News
Loading...

Advert

Thursday, June 16, 2016

Wanao pandisha bei ya bidhaa kutokana na misingi ya siasa kufutiwa lesseni zanzibar.soma zaid.


Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
imesema itawazuilia leseni
wafanyabiashara watakaobainika
kuwanyima huduma ama kuwapandishia
bei baadhi ya wananchi kutokana na
misingi ya kisiasa.
Akijibu suali la Mwakilishi wa viti maalum
Viwe Khamisi Abdallah, katika Baraza la
Wawakilishi Chukwani Zanzibar alietaka
kujua iwapo Serikali inafahamu suala la
hilo, Waziri wa Biashara, Viwanda na
Masoko Balozi Amina Salum Ali alisema
Serikali inalifahamu suala hilo na tayari
linafanyiwa kazi na wakuu wa wilaya.
Balozi Amina alisema katika kisiwa cha
Pemba kumekuwa na uchafuzi wa kisiasa
na baadhi ya wanasiasa wanatumia nafasi
hiyo kuwapandishia bei wananchi
hususan wanachama wa CCM.
Alisema wamekuwa wakichukua hatua ya
kuwafungia kwa muda mfupi
wafanyabiashara wenye tabia hiyo lakini
hivi sasa watawazuilia leseni kwa muda
wa mwaka mmoja kama adhabu na onyo.
Mapema akijibu suali la Mwakilishi wa
Jimbo la Fuoni Yussuf Hassan Iddi,
Balozi Amina alisema Seriksali inafanya
juhudi kubwa za kusimamia bei za bidhaa
muhimu ikiwemo,mchele,Unga wa
ngano,na sukari ili kuhakikisha hakuna
upandaji wa bei kiholela.
Alikiri kuwa baadhi ya bidhaa hizo
zimepanda bei kidogo kutokana na
kupanda mara kwa mara kwa thamani ya
Dola na kuongezeka kwa gharama
nyengine za biashara zikiwemo kuchelewa
kushusha mizigo bandarini.
Alisema Serikali imefanya juhudi kubwa
kupunguza tatizo la upandaji wa bidhaa,
ikiwemo kufanya mazungumzo na Shirika
la Bandari pamoja na Jumuiya ya
Wafanyabiashara Wenye Viwanda na
Wakulima (ZNCCIA) ili kutafuta ufumbuzi
wa suala hilo.
Aliongeza kuwa Wizara yake inaendelea
na juhudi ya kuhahikisha bidhaa muhimu
za chakula kwa ajili ya mwezi mtukufu
Ramadhani ikiwemo unga wa
ngano,Tende na Sukari vinapatikana kwa
bei nafuu ili kuwapunguiza mzigo
wananchi ndani ya mwezi huu.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top