Ajira za wasichana chini ya umri wa miaka 18 kupigwa marufuku.soma zaid.
Serikali imekusudia kutunga sheria ya
kupiga marufuku ajira za wasichana wa
kazi wenye umri chini ya miaka 18 kabla
ya mwisho wa mwaka 2016.
Hatua hiyo inaelezwa inakusudia kuinua
hadhi ya kazi na ajira za wasichana wa
kazi nchini, kwani muda wa kurasimisha
ajira hizo umefikia wakati wake.
Hayo yamebainishwa leo mjini hapa na
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy
Mwalimu wakati akizungumzia na
waandishi wa habari kuhusu maadhimisho
ya siku ya mtoto wa afrika
inayoadhimishwa tarehe 16 Juni kila
mwaka.
alisema hatua inachuliiwa na Serikali
kutokana na wasichana wengi wa ndani
kutumikishwa kazi hiyo katika umri
mdogo na kulipwa ujira mdogo.
“Tumepanga kutunga kanuni na sheria ya
kupiga marufuku ajira za wasichana wa
kazi wenye umri chini ya miaka 18, na
ndio maana tunawachukua katika umri
mdogo sana na kuwalipa ujira mdogo,
hivyo ukimchukua binti wa miaka 18
utaweza kuinua hadhi ya kazi ya kazi
yenyewe” alisema Waziri Ummy.
Akizungumzia kuhusu maadhimisho hayo,
Waziri Ummy aliitaka jamii kukataa
kurubuniwa kwa pesa na katika
kuwavichua watu wanaofanya vitendo vya
ukatili kwa watoto ikiwemo kulawiti na
kuwabaka na badala yake watoe taarifa
katika vyombo vya dola ili adhabu kali
zichuliwe dhidi yao.
Aidha Waziri Ummy aliwata wazazi nchini
kujenga tabia ya kukagua maumbile ya
watoto wao hususani watoto wa kike
ikiwemo kuwaogesha angalau mara moja
kwa mwezi, kwani kwa kufanya hivyo
kutamwezesha mzazi kufahamu afya ya
kimwili ya motto wake.
Kwa mujibu wa Waziri huyo alisema
vitendo vya ulawiti havifanywi kwa watoto
wa kike pekee bali na watoto wa kiume
pia wamekuwa wahanga wa vitendo hivyo,
ambapo ameitaka jamii kutowaamini
ndugu au jamaa zao kulala kitanda
chumba kimoja na watoto wao.
“Kwa mujibu wa taarifa za jeshi la Polisi,
vitendo hivi vimekuwa vikifanyika zaidi
majumbani kwa asilimia 49, asilimia 23
wakati wa kurudi na kwenda shule na
asilimia 15 wakiwa shuleni, hivyo kwa
takwimu hizi unaweza kuona ukubwa wa
tatizo ulivyo” alisema Waziri Ummy.
Chanzo: Michuzi
0 comments :
Post a Comment