Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, June 15, 2016

Rais Obama alia na Donard Trump.soma zaid.


Rais wa Marekani, Barack Obama, ameshtumu
vikali matamshi ya mgombea urais kwa tiketi ya
chama cha Republican, Donald Trump, kwamba
waislamu wasiruhusiwe kuingia Marekani.
Obama amesema hiyo 'si marekani wanayohitaji.'
''Kuwabagua Waislamu wa Marekani
kutasababisha nchi hiyo kukosa usalama,na
kuongeza tofauti iliopo kati ya nchi za magharibi
na zile za kislamu'', Obama alisema
Siku ya Jumatatu bwana Trump, aliongezea
kuhusu mpango wa kupiga marufuku nchi zote
ambazo zina historia ya kutekeleza mashambulizi
dhidi ya Marekani.
Alisema shambulio la ufyatuliaji risasi la Orlando
linathibitisha yote.
Watu 49 waliuawa, baada ya Omar Mateen raia
wa Marekani ambaye wazazi wake ni raia wa
Afghan kufyatua risasi katika kilabu ya wapenzi
wa jinsia moja huko Orlando.
Bwana Trump amesema pendekezo lake
litatekelezwa kupitia (uamuzi wa pamoja ) iwapo
rais atapewa mamlaka ya kupiga marufuku
uingizaji wa watu wenye daraja lolote katika nchi
hiyo jambo ambalo rais ataliona kuleta madhara
ya kiusalama kwa Marekani.
Lakini siku ya Jumanne katika wizara ya fedha
mjini Washington,Obama aliyekuwa
amekasirishwa na matamshi hayo ya Trump
alimshambulia mgombea huyo anayetarajiwa
kuthibitishwa kuwa mteuzi wa urais wa chama
cha Republican mwezi ujao.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top