Mume amnyonga mkewe kisa wivu wa mapenzi mkoan shinyanga.zoma zaid.
Huko Shinyanga mwanamke mmoja
aliyejulikana kwa jina la Rehema Tumbo
amenyongwa na mumewe Raphael
Kazembe tena kwa kutumia Khanga kisa
kikuu kikiwa ni wivu wa mapenzi.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa
Shinyanga Graiftoni Mushi, amethibitisha
kutokea kwa tukio hili, na inadaiwa kuwa
mwanamke huyo alichelewa kurudi na
alipomgongea mumewe chumbani
wanakolala hakumfungulia ndipo
alipoamua kwenda kulala katika chumba
cha watoto ndipo mwanaume huyo
alipoamua kufuata na kuanza kumpiga na
kumnyonga hatimae kumsababishia
mauti.
Mtuhumiwa alikimbia baada ya tukio hili
na mpaka sasa polisi wanaendelea na
juhudi za kusaka kokote aliko, Mwenyekiti
wa mtaa huo bwana Edward Mihayo
anasema taarifa zilimfikia kutoka kwa
wanamtaa waliomfuata kumwambia mara
baada ya kushuhudia maiti ya rehema
ikiwa imenyongwa kwa Khanga.
Sasa wanaJF, yaani wivu mpaka
usababishe mauti?
0 comments :
Post a Comment