Breaking News
Loading...

Advert

Sunday, July 17, 2016

Hakuna mtumishi yeyote atakaye kuwa na tenda serikalini.soma zaid.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI George
Simbachawene amesema serikali tayari
imekataza watumishi wa umma kujiingiza katika
kuomba tenda mbalimbali za serikali na
hawaruhusiwi na kama mtu anajihusisha na
jambo hilo basi anakiuka misingi ya sheria
Waziri Simbachawene ameyasema hayo kwenye
mahojiano maalumu na East Africa Radio
kuhusu baadhi ya watendaji wa umma ambao
wanamiliki kampuni ambazo zinashiriki kufanya
tenda ya serikali na zimekuwa zikifanya vibaya
na kusababisha malumbano baina ya wanachi
na halmashauri mbalimbali nchini.
Amesema wamezuia swala hilo kisheria ili
kuepuka usumbufu ambao umekuwa ukijirudia
mara kwa mara pindi serikali ifanyapo ukaguzi
wa utekelezaji wa kampuni hizo sambamba na
kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa wananchi
kuhusu utendaji kazi wa kampuni hizo, ambazo
zinakuwa zimepewa tenda na halmashauri
mbalimbali nchini.
Amewataka wakurugenzi na viongozi wa mikoa
kuzingatia sheria ya manunuzi inavyoelekeza na
tayari wameanza uchunguzi kuwabaini
watendaji wasio waaminifu juu ya swala hilo na
pindi watakapogundulika kuhusika na swala hilo
serikali itachukua hatua za kisheria.
Ametoa wito kwa watumishi wote wa serikali
kutokujihusisha na swala hilo na wazingatie
katika kusimamia haki na usawa kwa
watanzania ambao ndiyo walipa kodi na
watumiaji wa huduma mbalimbali za serikali.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top