Stika feki za TRA zatumika kuuzia kazi za wasanii.soma zaid.
Kampuni ya Msama Promotions imeeleza
kuwabaini maafisa wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania TRA wanaouza stika halisi za
mamlaka hiyo kwa ajili ya kutumika kuuzia
bidhaa bandia, ikiwemo kazi feki za sanaa.
Alex Msama, akionesha mbele ya waandishi wa
habari, stika za TRA ambazo hutumika kwenye
kazi feki za wasanii.
Hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku mbili baada ya
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
nchini Tanzania Mh. Nape Nnauye kutembelea
maduka ya kazi za sanaa katika soko la
Kariakoo jijini Dar es salaam na kubaini wauzaji
wa kazi feki za sanaa.
Akizungumza leo jijini Dar es salaam
mkurugenzi wa kampuni hiyo Alex Msama
amesema kuwa suala hilo ni sehemu ya jitihada
za kuunga mkono ukomeshwaji wa wahujumu
uchumi na wakwepa kodi nchini Tanzania.
Aidha Msama amempongeza waziri Nape na
kusema kuwa ni vyema watanzania wakafahamu
kuwa kinachohitajika sasa ni watu kufanya kazi
halali na sio kuwaibia wengine kwa njia tofauti
tofauti.chanzo muungwana.com
0 comments :
Post a Comment