Baada ya Mrema kuteuliwa na Rais afunguka haya.soma zaid.
Mwenyekiti wa TLP Dkt. Augustino Lyatonga
Mrema amesema Rais Dkt. John Magufuli
anaishi kwenye maneno yake kwa kuwa mwaka
jana alipofika kwenye jimbo la Vunjo aliwaambia
wananchi wamchague Mrema na
wasipomchagua atampa kazi, jambo ambalo
ametimiza
Mrema ameyasema hayo alipofanya mahojiano
maalum na EATV kuhusu uwezo wake wa
kusimamia Bodi ya Parole ambayo yeye ndiye
mwenyekiti wake baada ya kuteuliwa na Rais
Dkt. John Magufuli.
''Nafasi ambayo amenipa Rais Dkt. Magufuli
nina uzoefu nayo kwa kuwa mwaka 1994 njia
tuliyokuwa tunaitumia ni kutembelea magereza
na kuongea na wafungwa hasa wanaotumia
vyombo vya moto na wengine walikuwa
wanataja walipoficha silaha, na wengine
walikuwa wanataja wahalifu ndani ya jamii na
nilipata ushirikiano wa kutosha.''
Aidha Dkt. Mrema amesema anachokitafuta
Rais Dkt. John Magufuli ni mtu mzalendo na
hatua ya Rais kumteua ni kuonesha imani yake
kwake na si kwamba ana nia ya kuua upinzani
bali ana lengo jema la kuchukua mtu mwenye
uzoefu ili atumikie watanzania kwa sababu
lengo la upinzani siyo kutaka wananchi
wateseke.
''Watanzania wategemee ufanisi na kazi
iliyotukuka ya kupunguza wafungwa magerezani
ili waweze kupewa adhabu nyingine ndani ya
jamii na wapewe watu wa kuwasimamia, kwa
kuwa tatizo kubwa tulilonalo sasa hivi ni
mlundikano wa wafungwa na serikali haiwezi
kujitika kutanua magereza kwa kuwa sasa hivi
inajikita kuboresha huduma za afya na elimu
mfano suala la madawati'' Amesema Dkt.
Mrema
Kuhusu yeye kuwa mzee na kama ataweza
kumudu nafasi hiyo Dkt. Mrema amesema yeye
ana miaka 72 na hana uzee wowote ambao
utamfanya akwame kufanya kazi hiyo kwa
ufanisi na hata kabla ya uteuzi Rais ana watu
wa kumshauri na wameona anafaa nafasi hiyo
0 comments :
Post a Comment