Breaking News
Loading...

Advert

Sunday, July 17, 2016

Aliyekuwa mbunge wa CHADEMA jimbo la Longido Onesmo Ole Nangole amekata rufaa.soma zaid.

IKIWA zimepita siku chache baada ya
Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kumvua
Ubunge wa Jimbo la Longido, Onesmo ole
Nangole, sasa amekata rufaa, anaandika Faki
Sosi.
Nangole kupitia Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema) alitangazwa kuwa
mbunge wa jimbo hilo kwenye uchaguzi
uliofanyika tarehe 25 Oktoba mwaka jana.
Hivi karibuni mahakama hiyo imetengua Ubunge
wa Nangole kwa madai ya kugubikwa na kasoro
kadhaa na kudaiwa kuondoa uhalali wa yeye
(Nangole) kuendelea kushikilia nafasi hiyo.
Jaji Sivangilwa Mwangesi wa mahakama hiyo
alieleza kuridhishwa kwake na hali halisi katika
chumba cha kuisabia kura kwamba haikukidhi
matakwa halisi ya uisabuji wa kura.
Hatua ya kumvua ubunge Nangole imekuwa
ikipingwa na viongozi pia wanachama wa
chama hicho kwamba, haiakisi matakwa ya
kisheria na kwamba, jambo hilo halikubaliki.
Hata hivyo Nangole akiwa katika Jimbo la
Longido wakati akiwashukuru wananchi wa
jimbo hilo amesema kuwa, hakubaliana na
hukumu hiyo.
“Nimeishawasilisha maombi ya kukata rufaa”
anasema Nangole na kuongeza kuwa, maombi
hayo tayari yamepokewa.
Amesisitiza kuwa, madai ya kuwepo kwa
mazingira yasiyo rafiki ama kufanya fujo kabla
ya kutangazwa kwa matokeo hayana msingi
wowote na kwamba, kilichokuwa kikisimamiwa
ilikuwa ni madai ya kusimamiwa kwa haki.
Anasema, hatua hiyo ndiyo iliyowezesha
kutangazwa kwa matokeo kama yalivyokuwa
yakionesha na kwamba, tayari aliona kuwepo
kwa mazingira ya kutaka ‘kuchakachuliwa’ kwa
matokeo hayo.
“Kwa hakika hakukuwa na haki hata kidogo
katika hukumu,” amesema Nangole.
Kesi ya kupinga ubunge wa Nangole ilifunguliwa
na Dk. Stephen Keruswa, aliyekuwa mgombea
ubunge katika jimbo hilo kupitia Chama Cha
Mapinduzi (CCM).

0 comments :

Post a Comment

Back To Top