Wakurugenzi 6 NSSF wasimamishwa kazi.soma zaid.
BODI ya Wadhamini ya Shirika la Taifa la
Hifadhi ya Jamii (NSSF) imeagiza
kusimamishwa kwa wakurugenzi sita, mameneja
watano na mhandisi mmoja wa shirika hilo
kupisha uchunguzi, kubaini wahusika katika
tuhuma za ubadhirifu, matumizi mabaya ya ofisi
na kutofuata kanuni, sheria na taratibu katika
uwekezaji, usimamizi wa miradi, manunuzi ya
ardhi na ajira.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya NSSF,
Profesa Samwel Wangwe, alikiri jana usiku
kusimamishwa kwa vigogo hao 11, kupisha
uchunguzi wa tuhuma zilizoelekezwa kwao.
“Ni taarifa sahihi hizo. Kulikuwa na tuhuma katika
ripoti ya ukaguzi, kwa hiyo tumeamua wakae
pembeni ili kupisha uchunguzi, hawajafukuzwa
kazi. Taarifa hiyo ya kusimamishwa ni sawa
sawa,” alisema Profesa Wangwe jana usiku.
Kwa mujibu wa taarifa kwa wafanyakazi,
iliyotolewa na Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa
NSSF, iliwataja wakurugenzi sita
waliosimamishwa kuwa ni Yacob Kidula
(Mkurugenzi wa Mipango, Uwekezaji na Miradi),
Ludovick Mrosso (Mkurugenzi wa Fedha) na
Chiku Matessa (Mkurugenzi wa Rasilimali Watu
na Utawala).
Wengine ni Sadi Shemilwa (Mkurugenzi wa
Udhibiti Hadhara na Majanga), Pauline Mtunda
(Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Mahesabu ya
Ndani) na Crescentius Magori (Mkurugenzi wa
Uendeshaji).
Aidha, taarifa hiyo iliwataja mameneja
waliosimamishwa kuwa ni Amina Abdallah
(Meneja Utawala), Abdallah Mseli (Meneja wa
Uwekezaji), Mhandisi John Msemo (Meneja wa
Miradi), Davis Kalanje (Mhasibu Mkuu), Wakili
Chedrik Komba (Meneja Kiongozi – Mkoa wa
Temeke) na Mhandisi John Ndazi (Meneja
Mradi).
Taarifa hiyo kutoka Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu
wa NSSF, ilisema kwamba uamuzi huo
umefanywa na Bodi chini ya Profesa Wangwe
iliyokutana Julai 15, mwaka huu kutokana na
taarifa mbalimbali za wakaguzi wa hesabu na
shughuli za uendeshaji wa shirika hilo la umma.
“Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Taifa la Hifadhi
ya Jamii chini ya Uenyekiti wa Profesa Samwel
Wangwe katika kikao chake cha 106 kilichofanyika
tarehe 15 Julai, 2016 kimeagiza kusimamishwa
kazi kwa wakurugenzi sita (6), mameneja watano
(5) na mhandisi mmoja ili kupisha uchunguzi
kubaini wahusika katika tuhuma za ubadhirifu,
matumizi mabaya ya ofisi na kutofuata kanuni,
sheria na taratibu katika uwekezaji, usimamizi wa
miradi na manunuzi ya umma na ajira,” ilieleza
taarifa hiyo.
Hivi karibuni, NSSF ilitajwa katika vyombo vya
habari kuhusu tuhuma zikiwamo za ununuzi wa
ardhi usiofuata taratibu za manunuzi ya umma,
kuwapo kwa ubadhirifu na ajira za upendeleo
katika shirika hilo, ukiwataja wahusika kuwa ni
baadhi ya wakurugenzi wa shirika hilo.chanzo mpekuzi blog
0 comments :
Post a Comment