Udahili kupitia TCU kuanza kesho.soma zaid.
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), itaanza
kudahili wanafunzi waliomaliza kidato cha sita
wanaoomba kujiunga na vyuo vikuu kuanzia
kesho.
Akizungumza jana, Kaimu Mkurugenzi wa
Udahili na Nyaraka wa TCU, Dk Kokubelwa
Mollel alisema udahili kwa wenye diploma
utaanza Julai 31.
Dk Mollel alisema kazi hiyo itaendelea kwa
mwezi mzima ili kuruhusu wananchi wengi zaidi
kupata fursa ya kuomba kudahiliwa na udahili
huo utafanyika kwa njia ya mtandao.
Alisema ili wanafunzi waweze kuelewa
programu zinazotolewa na vyuo vikuu, tume
hiyo imeandaa maonyesho ya 11
yatakayofanyika kuanzia Julai 20 hadi 22,
mwaka huu.
Alisema maonyesho hayo yatafanyika katika
viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam na
kufunguliwa na Waziri wa Elimu, Sayansi,
Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce
Ndalichako.
0 comments :
Post a Comment