Baada ya zoezi la madawati kukamilika sasa ni vyumba vya madarasa.soma zaid
Waziri mkuu Kasimu Majariwa amesema baada
ya zoezi la kutengeneza madawati kukamilika
kwa asilimia kubwa ni wakati sasa wa
kuelekeza nguvu katika ujenzi wa vyumba vya
madarasa ili kukabiliana na tatizo la wanafunzi
kusomea chini ya miti wakiwa wanakaa kwenye
madawati yaliyotengenezwa.
Waziri mkuu amesema hayo wakati
akiziungumza na wakuu wa wilaya,wakurugenzi
pamoja na watendaji wengine wa halmashauri
za mkoa wa Mtwara ambapo amesema katika
kukabiliana na changamoto za elimu bure
utekelezaji wa madawati kwa shule za msingi
umefanikiwa kwa asilimia 88.8 na kwa shule za
sekondari ni asilimia 95.8.
Akizungumza na viongozi pamoja na watendaji
wa wilaya na halmashauri za mkoa wa Mtwara
waziri mkuu kasimu Majariwa amesema
kutokana na muitikio mkubwa wa wazazi
kuwapeleka watoto shule uhaba wa vyumba vya
madarasa umeongezeka na serikali isingependa
kuona madawati yaliyotengenezwa yanakaliwa
na wanafunzi chini ya miti hivyo viongozi wa
wilaya wanapaswa kuelekeza nguvu katika
ujenzi wa vyumba vya madarasa.
Aidha amewataka wakurugenzi walioteuliwa
kuhakikisha maeneo ya shule yanapimwa na
kupatiwa hati miliki ili kuepuka uvamizi na
migogoro ya ardhi inayoibuka kutoka kwa
wananchi wavamizi wa maeneo.
0 comments :
Post a Comment