Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, July 20, 2016

Mugabe ataongoza mpaka atakapo fariki..soma zaid.

Kiongozi mmoja wa vijana katika chama tawala
nchini Zimbabwe Zanu-PF amesema watu
wasitarajie kwamba Rais Robert Mugabe,
atastaafu.
Kiongozi huyo Kudzai Chipanga amesema Bw
Mugabe, mwenye umri wa miaka 92 ataongoza
kwa umri wake wote hadi atakapofariki.
Aidha, amesema: "Hata kwenye Biblia
imeandikwa hivyo kwamba Mugabe, atawala hadi
atakapofariki ''.
Ameyasema hayo alipokuwa akiwahutubia
wafuasi wa chama hicho wapatao 5,000 katika
mkutano wa kisiasa mjini Harare.
Hatua hiyo ni kama majibu kwa upinzani nchini
humo ambao umekuwa ukiendesha kampeni
inayoonekana kuenea kupitia mitandao ya kijamii
ikitumia kitambulisha mada #ThisFlag, maana
yake Bendera Hii.
Mugabe: Aliyeongoza maandamano sio
mhubiri wa kweli
Kampeni hiyo imekuwa ikiendelezwa na kasisi
mmoja aitwae Pastor Evan Mawarire:
Akiendelea kueleza kukasirishwa kwake na
kampeni hiyo Chipanga ameongeza kusema:
“Hamna kokote ilikoandikwa kuwa eti ‘Kasisi
ataitawala Zimbabwe”.
Ameyataka maandamano hayo ya wapinzani
yakome mara moja.
''Sisi hapa Zanu-PF, tulipambana na wakoloni
hadi 1980 na tukawashinda, bado ndio
tunatawala hapa na hamna kitakachobadilika,”
akasema Bw Chipanga
Jana Robert Mugabe mwenyewe, ambaye
amekuwa madarakani tangu 1980, alimshutumu
Kasisi Evan Mawarire, ambaye amekuwa
akimkosoa Rais Mugabe akimlaumu kwa
kuporomoka kwa uchumi wa Zimbabwe na
kumtaka ajiuzulu.
Mwezi jana Kasisi Mawarire, aliongoza mgomo
mkubwa wa kumpinga Mugabe ambapo
wafanyakazi waligoma kufika kazini siku hiyo.
Mshirikishe mwenzako Unavyoweza
kumshirikisha mwenzako

0 comments :

Post a Comment

Back To Top