Mwanamke aisaliti ndoa yake kwa usaliti.
Kuna picha zinasambaa kwenye mitandao ya
kijamii zikimuonesha mwanamke akifanya
mapenzi na mpenzi wake. Yote hayo yalitokea
siku chache tu baada ya mwanamke huyo
kufunga ndoa na mwanaume mwingine jijini Dar
es Salaam.
Mwanamke huyo amedai kuwa picha hizo
alijipiga na mpenzi wake zamani miaka saba
iliyopita wakiwa chuoni na zimekuja kusambaa
ndani ya wiki baada ya kufunga ndoa. Anadai
kuwa ni kisasi cha ex wake aliyedhamiria
kuivunja ndoa yake.
Akiongea kwenye Ripoti ya Siku ya kipindi cha
Ubaoni cha EFM kilichoruka Ijumaa iliyopita,
mwanamke huyo amedai kuwa picha hizo
zimedhamlilisha mno kiasi cha kuiharibu ndoa
yake, kuwaumiza ndugu zake na kuwakosea
heshima wakwe zake na kwamba anajuta kupita
kiasi.
“Ni kweli ni mimi ndiye niliyepiga hizo picha lakini
ni muda mrefu tangu kipindi nikiwa chuo, yaani
hata huyo mtu mwenyewe sijui yuko wapi sina
mawasiliano naye tena, sikutegemea kiukweli,”
anasema mwanamke huyo.
“Ni kitu ambacho kinaniuma na kimeniharibia
mlolongo mzima wa maisha yangu, mpaka sasa
hivi sielewi, mume wangu hawezi kunielewa tena
na yeye ndio nimemwekea kama nguzo, ndio kila
kitu kwasababu hata familia yangu hainielewi ,”
ameongeza.
“Mpaka sasa hivi sijui nafanya nini.”
Kwa upande wa mume wake, alidai kuwa picha
hizo zimeuvunja moyo wake.
“Tulikuwa tumeshaenda kwenye honey moon
tumerudi, sikuamini macho yangu baada ya kuona
hizo picha na huyu mwanamke, rafiki zangu
walikuwepo wengi sana, best man wangu pia ni
vitu ambavyo kuvizungumza mimi nashindwa,
naanzia wapi, lakini mapenzi huwa yako hivyo,
inawezekana iko hivyo lakini sasa kama mazingira
kama yale hata kama ukiwa ni wewe lazima
utaumia, familia yangu ntaiambia nini mimi,
imenigharamia harusi kubwa,” alisema
mwanaume huyo.
Amedai kuwa haoni kama inawezekana tena
kukaa chini na mke wake huyo kwa kile
kilichotokea.
“Nikae chini ili iweje?” alihoji kwa jazba.
“Imeniuma, imeniumiza sana hii kitu haki ya
Mungu, hata kama miaka kumi imepita kwanini
imekuja kwenye harusi yangu, zawadi zimekuja
kwaajili ya harusi yetu kwanini aletewe picha za
aina hiyo? Angeniambia before kwamba nilikuwa
na moja mbili, ningekuwa najua, lakini
amenificha. Imenicost kwa kiasi kikubwa sana,
nitaiambiaje familia yangu kwa mfano? Nitasema
nini.”
“Sitokuja kupenda tena mwanamke wa aina yoyote
ile, mpaka nakuja kuingia kaburini, I swear to
God, imetosha kabisa.”
Wawili hao walifunga ndoa tarehe April 23
mwaka huu.
Kwa mujibu wa best man wa harusi hiyo,
waliziona picha hizo siku nne baada ya harusi
wakati wanafungua zawadi walizopewa na
kuzikuta zikiwa kwenye bahasha na kusababisha
vita kubwa kwenye familia yao.
Anadai kuwa rafiki yake hataki kusikia chochote
kuhusiana na kumsamehe mke wake na jitihada
za ndugu kuwasuluhisha zimegonga mwamba.
“Yaani hapo alipo nakuambia haelewi, mtu
anayenisikiliza ni mimi tu, hasikilizi mtu yeyote.
Huyo mwanamke ndio analia muda wote, jamaa
haelewi,” amesema best man huyo
aliyejitambulisha kwa jina la Geofrey Nicholas.
Sikiliza mkasa mzima hapo chini.
0 comments :
Post a Comment