Breaking News
Loading...

Advert

Tuesday, July 19, 2016

Rushwa huchochea migogoro ya Ardhi nani kasema?.soma zaid.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Dkt Angeline
Mabula ayataka Mabaraza ya Ardhi na
Nyumba kuepuka rushwa kutoka kwa
wenye fedha kwa kuwapa upendeleo na
kukandamiza wanyonge katika maamuzi
yahusuyo migogoro ya ardhi.
Angeline ameyasema hayo wakati
alipofanya ziara ya kutembelea Baraza la
Ardhi na Nyumba la Tanga mjini. Wakati
wa ziara hiyo Naibu Waziri amepiga
marufuku tabia ya baadhi ya watu ambao
huwapa pesa waendesha mashtaka na
wenyeviti wa mabaraza ya Ardhi na
nyumba ili kupindisha sheria.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline
Mabula akipekua mafaili ya hukumu za
migogoro ya ardhi ili kujiridhisha kama
haki inatendeka kwa wananchi wakati
alipotembelea Baraza la Ardhi na Nyumba
la Tanga mjini.
Naibu Waziri wa Ardhi, Dkt Angeline
Mabula akiongea na watendaji wa Baraza
la Ardhi na Nyumba la Tanga mjini.
Baadhi ya watendaji na watumishi wa
umma wakimsikiliza Naibu Waziri wa
Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
Dkt Angeline Mabula katika ofisi za
Baraza la Ardhi na Nyumba la Tanga
mjini.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top