Breaking News
Loading...

Advert

Tuesday, July 19, 2016

Mkuu wa mkoa wa Dar Paul makonda ametolea ufafanuzi kauli yake.soma zaid.

Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Paul Makonda ametoa ufafanuzi wa
shughuli ya sensa ili kubaini watu wasiokuwa na
kazi, akisema hajatamka wasio na kazi
wakamatwe.
Akihojiwa jana katika kipindi cha Power Breakfast
kinachorushwa na Redio Clouds, Makonda
alisema watu hawakuelewa lengo la sensa hiyo.
Makonda alisema lengo la kuwatambua watu
wasiokuwa na kazi ni kwa ajili ya kuimarisha
ulinzi na usalama katika Mkoa wa Dar es
Salaam.
Alisema anacholenga katika sensa hiyo, ni kwa
ajili ya usalama wa mkoa ili kila mtu ajulikane
shughuli anayoifanya. Aliongeza kuwa
ameshangaa kusoma kwenye mitandao ya jamii,
watu wakijadili mambo ambayo hajawahi
kuyatamka.
Makonda alisema alipoteuliwa na Rais John
Magufuli kuwa mkuu wa mkoa na mwenyekiti wa
kamati ya ulinzi na usalama, alifanya mkutano na
wenyeviti wa mitaa.
Alisema katika mkutano huo, aliwaeleza
wenyeviti hao kuwafahamu vizuri watu kwenye
mitaa wanayoiongoza, akiwataka wajue kazi
wanazozifanya wananchi wao kwa ajili ya
usalama.
Tangu kuibuka kwa sakata hilo, kumekuwa na
majadiliano yanayoendelea katika mitandao ya
jamii kuhusu kauli ya Makonda ya msako wa
nyumba kwa nyumba kuwabaini vijana
wasiokuwa na kazi, huku wengi wao
wakilalamikia tamko hilo.
Kuhusu kuondoa ombaomba, Makonda alisema
ataendelea na kazi hiyo ili watoto wanaoomba
wajiunge na shule za msingi.
“Rais John Magufuli ametoa nafasi kwa watoto
hawa kusoma bure, lakini wao wapo barabarani
wanaomba, hivi kuwapa fedha ni kuwasaidia?”
alihoji.
Makonda alisema watoto wengi wanatumikishwa
katika kazi ya kuomba na watu ambao siyo
ndugu zao.
“Yaani wao wanaomba lakini mtu mwingine ndiye
anachukua fedha hizo, natoa wito jamii inisaidia
kwa kutowapa fedha ombaomba hawa,” alisema
Makonda. Alisema shughuli ya kuwaondoa ilianza
Juni na kwamba mwezi ujao atatoa tathmini ili
kuona kama imefanikiwa au la.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top