Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, March 23, 2016

Mkurugenzi manispaa kigoma ujiji apewa siku moja kutoa maelezo kuhusu upotevu wa sh.bilion 2.46.soma zaid.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais utumishi na utawala
bora Mh.Angella Kairuki ametoa siku moja kwa
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji na
Mkoa kutoa maelezo ya matumizi ya shilingi
bilioni 2.46 zilizotolewa na Serikali katika mwaka
wa fedha 2014/2015 kwa ajili ya kugharamia
ujenzi wa nyumba za Walimu,Vyoo na usimamizi.
Waziri Kairuki ametoa maagizo hayo jana baada ya
kamati ya Bunge ya utawala bora na Serikali za
mitaa kutembelea Shule ya Sekondari Kirugu
kata ya majengo mjini kigoma na kukagua baadhi
ya vyumba vya Madarasa vilivyojengwa na
mpango wa maendeleo ya jamii TASAF awamu
ya pili ambapo ilibainika kuwa shule hiyo haina
Nyumba za Walimu,jengo la utawala,umeme na
vyoo havitoshelezi,ambapo amesema hali hiyo
inaonyesha jinsi fedha zilizotolewa na serikali
hazikutumika kwa malengo yaliyokusudiwa katika
mkoa wa Kigoma na kutaka taarifa hiyo
iwasilishwe haraka kwa Waziri wa TAMISEMI
Mh.George Simbachawene.
Katika taarifa yake kwa kamati ya Bunge,ambayo
pia ilitembelea miradi ya barabara na kituo cha
mabasi mjini Kigoma zilizojengwa kwa msaada
wa Benki ya Dunia,Afisa mtendaji wa mtaa wa
Katonyanga kata ya Majengo Kilinako Iddi
amesema baada ya TASAF kujenga madarasa
shule imebakiwa na changamoto za umeme,
maji,nyumba za walimu,jengo la utawala na vyoo
huku Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya utawala
bora na serikali za mitaa Mh.Jasson Rweikiza
akiiomba TASAF kusaidia miundombinu ya maji
katika shule hiyo.chanzo itv.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top