Breaking News
Loading...

Advert

MICHEZO

MICHEZO

BURUDANI

BURUDANI

SIASA & JAMII KWA UJUMLA

SIASA & JAMII KWA UJUMLA

Recent Post

Sunday, November 26, 2017
Mwanafunz yatima ajinyonga kisa amefari mtihani chuo.soma zaid

Mwanafunz yatima ajinyonga kisa amefari mtihani chuo.soma zaid

Dar es Salaam. Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Udaktari cha Imtu, Daniel Mabisi (28) anadaiwa kujinyonga kutokana na kufeli mitihani. Mabisi ambaye ni mkazi wa mtaa wa Mgeninani, Kata ya Kijichi wilayani anadaiwa kukutwa amejinyonga jana saa saba mchana maeneo ya Mgeninani. Taarifa zilizopatikana zinadai siku mbili kabla ya kujinyonga, mwanafunzi huyo alionekana mtaani hapo baada ya kutoka chuo alikokuwa akisoma. Inaelezwa kuwa mwanafunzi huyo amefeli mara mbili mfululizo. Akizungumza kwa simu kutoka Morogoro, baba mdogo wa marehemu, Joseph Lukuba alisema amepokea kwa mshtuko taarifa za mtoto wake. “Nimepigiwa simu mchana huu nikaambiwa Daniel amejinyonga, nimeshtuka kwa sababu ni juzi tu tulimtumia nauli ili arudi nyumbani Mwanza baada ya kupata taarifa kuwa amefeli kwa mara nyingine,” alisema Lukuba. Alisema uamuzi aliouchukua unasikitisha kwa kuwa kufeli, isingekuwa sababu ya kushindwa maisha hadi kufikia uamuzi wa kujinyonga. “Kama familia tumehama na tuko mbali kikazi, tumemuomba jirani asimamie suala hili wakati taratibu za mazishi au kusafirisha mwili zikiendelea,” alisema. Akizungumzia tukio hilo, mwenyekiti wa Mtaa wa Mgeninani, Khuruka Mwinyimvua alisema baada ya kupata taarifa hizo alifika eneo la tukio na kukuta mwili ukiwa umening’inia juu ya mwembe. “Kijana huyo alionekana tangu juzi akizunguka mtaani hapa baada kurejea kutoka chuoni anakosoma, alionekana kama mtu asiyekuwa na furaha,” alisema Mwinyimvua na kuongeza: “Hadi sasa mwili umechukuliwa na polisi kwa taratibu nyingine.” Naye kamanda wa polisi Mkoa wa Temeke, Emmanuel Lukula alithibitisha kupokea taarifa za kujinyonga kwa kijana huyo na kuwaagiza askari walio karibu na maeneo hayo kuchukua mwili huo.chsnzo mwananch
KILOSA: Mtu mmoja amefariki kwa kufukiwa na kifusi.soma zaid

KILOSA: Mtu mmoja amefariki kwa kufukiwa na kifusi.soma zaid

Mtu mmoja mkazi wa Kitongo cha Rose kata ya Magomeni wilayani Kilosa mkoani Morogoro aliyejulikana kwa Jina la Salum Omary (37) amefariki dunia papo hapo baada ya kufukiwa na kifusi cha mchanga alipokuwa akijaribu kufanya shughuli za kuchimba mchanga katika shimo na kisha kufukiwa. Mwili wake umeokolewa na wananchi mara baada ya kupata tarifa za tukio hilo kwa watoto waliopita katika eneo hilo. 

Friday, November 24, 2017
MISRI:Takribani watu 155 wamefariki dunia baada ya Msikiti kushambuliwa kwa bomu huko Sinai.soma zaid

MISRI:Takribani watu 155 wamefariki dunia baada ya Msikiti kushambuliwa kwa bomu huko Sinai.soma zaid

MISRI: Takribani watu 155 wameuawa na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa kwenye shambulio la bomu na bunduki lilofanywa na watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa Kiislam kwenye msikiti wa al-Rawda uliopo mji wa Bir al-Abed wakati wa swala ya Ijumaa ======= Egyptian state news agency says death toll in Sinai mosque attack rises to 115, with 120 injured. ======= Suspected militants have launched a bomb and gun attack on a mosque in Egypt's North Sinai province, killing 85 people, the state news agency says. Witnesses told Egyptian media it happened in the town of Bir al-Abed near al-Arish during Friday prayers. Local police said men in four off-road vehicles opened fire on worshippers, AP reported. Egypt has been fighting an Islamist insurgency in the region, which has intensified since 2013. Some 80 people were also wounded in the attack, health officials said. One report said the target appeared to be supporters of the security forces who were praying at the mosque. President Abdul Fattah al-Sisi is to meet security officials to discuss the incident, Egypt's private Extra News TV reported. It is not yet known who was behind Friday's attack. Jihadist militants have been waging an insurgency in recent years, stepping up attacks after Egypt's military overthrew Islamist President Mohammed Morsi in July 2013. Hundreds of police, soldiers and civilians have been killed since then, mostly in attacks carried out by Sinai Province group, which is affiliated to so-called Islamic State (IS). Source: BBC

Friday, November 17, 2017
kwenye saluni nyingi za wanawake,mazungumzo mengi yanahusu maisha ya watu na  hasa kuhusu mapenzi na kipato,kashfa na saikologia zisizo rasimi kuhusu ndoa na mahusiano, je nikweli?

kwenye saluni nyingi za wanawake,mazungumzo mengi yanahusu maisha ya watu na hasa kuhusu mapenzi na kipato,kashfa na saikologia zisizo rasimi kuhusu ndoa na mahusiano, je nikweli?

Kwenye Saluni nyingi za wanawake, mazungumzo mengi yanahusu maisha ya watu na hasa kuhusu mapenzi na kipato, kashfa na saikolojia zisizo rasmi kuhusu ndoa na uhusiano. Kuna mazungumzao ya kukatishana tamaa na kuumizana zaidi, kwa sababu kila mmoja anajaribu kuonyesha kwamba ana nafuu fulani. Lakini mbaya zaidi ni kwamba, saluni za wanawake hutumiwa na wanawake hao kama maeneo ya kusemea hisia zao chungu na kutoa jumuisho kuhusu wanaume na uhusiano. Huko saluni hakuna wataalamu, bali kuna wazungumzaji ambao wanaamini wao ni wataalamu, na wengine kwa sababu ya kuzidiwa na mzigo wa matatizo hasa ya uhusiano na pengine ya kipato, huwaaamini hao wataalamu wasio rasmi. Huko saluni ndiko ambako wanawake wanaambiana`kwamba, mwanaume akiacha kufanya tendo la ndoa kwa wiki moja na mpenzi wake, ni lazima mwanaume huyo atakuwa na ‘nyumba ndogo.’ Ndiko ambako wanafundishana kwamba, ukipata Mganga wa nguvu unaweza kumshika mwanaume. Ndiko huko ambako hutajwa orodha ya wanawake ambao wamewashika waume zao kupitia kwa waganga. Ndiko huko ambako majina ya waganga maarufu hutajwa. Lakini ndiko huko saluni ambako, wanawake hutaja orodha ya wanawake wenzao waliopata mali kupitia ‘mabuzi,’ ambao huwapa mitaji ya biashara inayowawezesha kusafiri hadi Uchina. Pia hutajwa majina ya wanaume wanaohonga sana. Ni saluni ambako wataalamu wasio rasmi hutoa suluhu ya matatizo ya ndoa. Ndiko ambako wataalamu hao huwaambia wanawake wenzao kwamba, ukimuonyesha mwanaume kwamba unampenda sana, atakudharau na kukuacha. Kwa hiyo mwanamke akitoka saluni anakuwa ametoka shule anayoiamini . ambapo huacha kumwonesha mumewe kwamba, anampenda. Ni wazi shule hii ya saluni haijui kwamba, unapoonesha kutokupenda, nawe utaoneshwa kutokupendwa. Kwani unachopanda ndicho unachovuna. Wakati mwingine shule hii inajua jambo hilo, isipokuwa inataka waliopotea na kuharibikiwa wawe wengi. ⬅⬅⬅⬅⬅ Ni huko saluni ambako utasikia wanawake wakifundishana namna ya kuwadanganya wanaume zao. Hufundishana namna ya kujenga nyumba bila kunaswa na mume, kwani wanaume hawaaminiki, huwezi kuacha kujiandaa. Lakini shule hii haijui kuwa, hiyo ni sumu kubwa kuliko sumu nyingine kwenye ndoa, kutafuta mali na kujenga msingi wa kipato kwa siri. ⁉⁉⁉⁉⁉⁉ Ni hukohuko saluni ambako wanawake huambiana uongo kuhusu wakwe, watoto wa kambo, na mawifi. Hufundishana kwamba, kumpenda mama mkwe au wifi ama mtoto wa kambo ni kutafuta muhali. Haiishia hapo huendelea kufundishana hata namna ya kuwachukia watu hao. Mwanaume, kama ukiona mwenzi wako anakwenda saluni na akitoka huko amekuwa mtu mwingine kabisa, unapaswa kujua kwamba, huenda amepata ‘dozi’ ya wataalamu hao. Wanawake, nawashauri jihadharini sana na maneno ya saluni. Kwani katika kila maneno mia moja, ni moja tu linalokaribia ukweli. Kumbuka, linalokaribia ukweli . siyo kuwa ni la kweli……

Wednesday, November 15, 2017
Rais magufuli ameagiza kubomolewa kwa makao makiu ya TANESCO na wizara ya Maji.soma zaid

Rais magufuli ameagiza kubomolewa kwa makao makiu ya TANESCO na wizara ya Maji.soma zaid

Rais Magufuli leo atembelea Mradi wa Ujenzi wa Barabara za Juu za Ubungo unajulikana kaka ‘Ubungo Interchange’.  Aidha meagiza kuwa jengo la makao makuu ya Shirika la la Uzalishaji na Ugavi wa Umeme nchini TANESCO lililopo eneo hilo pamoja na jengo la wizara ya maji ambalo liko mkabala na jengo la TANESCO, yawekwe alama ya ‘X’ ili yabomolewe kupisha mradi huo.

Tuesday, November 14, 2017
SUMATRA: Marufuku abiria kuzungumza siasa,dini'biashara ndani ya basi.soma zaid

SUMATRA: Marufuku abiria kuzungumza siasa,dini'biashara ndani ya basi.soma zaid

Usimamizi wausafiri wa nchi kavu na majini (SUMATRA) imepiga marufuku abiria kuzungumza masuala ya siasa, dini na kufanya biashara wawapo safarini. Agizo hilo limetangazwa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA, Lingadi Ngewe na kwamba abiria atakayebainika kufanya vitendo hivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake. Agizo hilo linakuja baada ya hivi karibuni kudaiwa kuwapo kwa mvutano wa kupinga kanuni mpya kati ya Sumatra na chama cha wamiliki mabasi yaendayo mikoani (TABOA) na wa usafiri Dar es Salaam (UWAMADAR). Bila kutaja ni sheria na kanuni ipi, Mkurugenzi huyo amesema ufanyaji wa vitendo hivyo katika mabasi ni kinyume na kanuni za usafirishaji. "Tutaanza kuzuia wasafiri wa wapo ndani ya mabasi kuacha kuzungumza masuala ya siasa, dini na kufanya biashara. Tukibaini hilo hatua za kisheria zitachukuliwa kwa abiria na dereva ikibidi," amesema na kuongeza ‘Kwa madereva hasa wa kwenda mikoani, njiani wanapandisha wafanyabiashara na kufanya biashara ndani ya basi, hatua kali zitachukuliwa kwa dereva na huyo anayefanya biashara.’ chanzo jamii forums

Thursday, November 9, 2017
Wakili feki adakwa Dar.soma zaid

Wakili feki adakwa Dar.soma zaid

DAR: Wakili feki aliyetambulika kwa majina ya Bw. Jeremiah Ragita amekamatwa Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi. >Yadaiwa amebainika baada ya kusalimia Jaji "Shikamoo"  ​ ===== Pichani hapo juu ni Bw. Jeremiah Ragita aliyejifanya kuwa Wakili akitokea Kampuni ya Sheria ya Faithful Attorney Advocates kwa mujibu wa Naibu Msajili, Mahakama ya Ardhi, Mhe. Frank Mahimbali anasema Wakili huyo feki alikamatwa mapema Novemba 08 katika Mahakama hiyo akimsimamia Mleta maombi Nunu Mhusin Mkwata. Mhe. Mahimbali anasema kuwa upande wa pili ambao unasimamiwa na Wakili Maros Gabriel kutoka Kampuni ya Sheria ya 'Common Law Chambers' ulimtilia shaka Bw. Jeremiah Ragita kama kweli ni Wakili ndipo alipofanya upekuzi kwenye Ofisi ya TLS na kuambiwa kuwa hawana jina hilo. Hata hivyo Mhe. Mahimbali alienda mbali na kumuandikia barua Msajili wa Mahakama Kuu (RHC) na kujibiwa kuwa hakuna Wakili aliyesajiliwa kwa jina hilo. Kwa mujibu wa Naibu Msajili kesi hiyo ilipoitwa mbele ya Mhe. Jaji Crencesia Makuru, Wakili Maros alimueleza Mhe. Jaji kuwa mwenzake wa upande wa pili sio Wakili na kisha akatoa vielelezo kutoka katika Ofisi ya Msajili Mahakama Kuu na Ofisi ya TLS ndipo Bw. Ragita akakiri kuwa yeye si Wakili. Hata hivyo Bw. Ragita alikamatwa na kupelekwa Polisi Kituo cha Kati (Central Police) jijini Dar es Salaam kwa ajili ya hatua stahiki za kisheria. Mahakama inapinga vikali vitendo vya ulaghai (Mawakili feki, vishoka) vinavyofanywa na baadhi ya Wananchi kwa lengo la kujipatia kipato. - Mtazamo News
Back To Top