Au wapeleka wanajeshi 100 kurinda amani burundi.soma zaid.
Umoja wa Afrika umetangaza kwamba
utawapeleka waangalizi 100 wa haki za
kibinaadamu pamoja na waangalizi wengine 100
wa kijeshi nchini Burundi.
Umesema kuwa rais wa taifa hilo Pierre
Nkurunziza ameunga mkono mpango huo.
Rais wa Afrika kusini Jacob Zuma aliongoza
ujumbe wa viongozi watano wa Afrika katika
ziara ya siku mbili wiki hii.
Walikutana na bwana Nkurunziza na viongozi
wawili wa upinzani ambao wamesalia nchini
humo hata baada ya ghasia zilizozuka mwezi
Aprili baada ya Nkurunziza kutangaza kuwa
atawania muhula wa tatu.
Wamesema kuwa mpatanishi wa AU rais
Museveni wa Uganda ataanzisha mazungumzo
hivi karibuni.
Mshirikishe mwenzako Unavyoweza
kumshirikisha mwenzako.chanzo bbc swahili.
0 comments :
Post a Comment