Mawazir 4 na naibu wazir mmoja wapewa masaa 12 kujaza na kurudisha form za maadili.
Rais John Pombe Magufuli ametoa muda
mpaka leo jioni kwa Mawazri wa 4 na
Naibu waziri 1 ambao hawajarejesha fomu
kwa Sekretarieti ya maadili kwa ajili ya
kuanisha mali na madeni wanayodaiwa
ambapo wamepewa muda mpaka saa 12
wawe wamesharejesha fomu hizo.
Waziri mkuu Kassim Majaliwa amewataja
majina mawaziri hao kuwa ni
Agustine Mahiga
Charles Kitwanga,
January Makamba,
Joyce Ndali Chako na
Naibu waziri Mh.Luhaga Mpina.
=======
Waziri mkuu wa Jamhuri ya muungano wa
Tanzania, Kassim Majaliwa leo Jumanne
Februari 26, 2016 ameongea na
waandishi wa habari kuhusu kadhia ya
baadhi ya mawaziri wa serikali ya awamu
ya tano kushindwa kuresha fomu za hati
ya mali ya wanazomiliki. Kwanza alielezea
sekretarieti ya maadili na nini wajibu wake
ikiwemo kufatilia maadali ya viongozi wa
umma na sheria inayowataka viongozi
husika kutoa tamko la mali ndani ya siku
thelathini tangu uteuzi wao.
Majawaliwa: Viongozi wanaoshindwa
kutoa tamko katika kipindi kilichowekwa
kwa mujibu wa sheria wanawajibika kutoa
maelezo ya sababu za msingi za
kushindwa kwao kuwasilisha fomu hizo
za tamko la rasilimali na madeni
waliyonayo.
Endapo maelezo hayo hayatakuwa na
sababu za msingi, hatua zaidi za kisheria
huwa zinachukuliwa. Aidha viongozi wa
umma wanawajibika kusaini hati za
maadili, ahadi ya uadilifu kwa viongozi
wote wa umma. Zoezi hili lilianza mwaka
2015 na ni endelevu na lilikuwa na lengo
la commitment ya kiongozi juu ya uadilifu
wake wakati wote anapokuwa kiongozi wa
umma na tayari watumishi wengi wa
umma wanaendelea kuzijaza fomu hizo na
ndio msingi wa uwajibikaji katika sekta ya
umma.
Kwa misingi hiyo, mawaziri bado
wanaendelea na zoezi hilo lakini pia mtu
toka alipoteuliwa. Fomu hizo
walishakabidhiwa na wanawajibika
kurudisha tume.
Jana nilikabidhiwa majina ya mawaziri na
manaibu mawaziri ambao hawakuweza
kurudisha fomu zote mbili au fomu moja.
Na alikuwa analikuwa anatakiwa pia watoe
tamko la rasilimali walizonazo na madeni
waliyonayo na fomu hizo walitakiwa
kurejesha kwa kamishna.
Mhashimiwa Rais wa Jamhuri ya
muungano wa Tanzania ameelekeza
kwamba waziri na manaibu waziri wote
ambao hawajajaza tamko la rasilimali na
madeni, ifikapo leo Ijumaa saa kumi na
mbili jioni wawe wameshajaza na
kurejesha fomu hizo ofisi ya tume ya
maadili hapa Dar es Salaam.
Kwa waziri yeyote ambae atashindwa
kutekeleza agizo hilo atakua amejiondoa
mwenyewe kwa majukumu aliyonayo ya
uwaziri au unaibu waziri. Na mheshimiwa
Rais ameelekeza lazima wasomwe ili
popote walipo warudi na watekeleze hivyo
na ofisi yangu itasimamia kwa ukaribu
kuona kwamba fomu hizo zinapatikana
ifikapo saa 12.
Nao ni wafuatao, kundi la mawaziri
1. Charles Kitwanga(Waziri wa
mambo ya ndani, yeye hajarejesha
fomu zote mbili)
2. January Makmba (Hajarejesha
fomu zote mbili)
3. Dr Augustine Mahiga (Waziri wa
mambo ya nje, Fomu moja ya
maadili)
4. Prof Ndalichako (Fomu moja ya
tamko)
Manaibu
1. Luhaga Mpina (Mazingira na
muungano, hajajaza fomu zote
mbili)
===================
Update
Agizo la Rais Magufuli laanza
kutekelezwa, Waziri Mahiga arudisha
Fomu wengine wang'aka
Baada ya Waziri Mkuu kutaja majina ya
mawaziri wanne na Naibu waziri mmoja
ambao hawajarudhisha fomu za
Sekretariati ya maadili ya umma na
kutakiwa wawe wamerejesha fomu hizo
mpaka saa kumi na mbili jioni ijumaa ya
leo mpaka sasa ni waziri mmoja aliyetii
agizo hilo.
Aliyerudisha fomu hizo ni waziri wa
mambo ya nje,ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mhe.
Balozi dkt. Augustine Mahiga ambapo
amekiri kuwa ni kweli alikuwa hajarudisha
fomu hizo kutokana na majukumu ya kazi
yaliyokuwa yamembana.
ITV pia imefanikiwa kuongea na waziri wa
mambo ya ndani Charles Kitwanga
ambaye naye ametajwa kutorudisha fomu
hizo ambapo ameshangaa jina lake
likitajwa wakati ameshazirudisha na kwa
sasa ameelekea ofisi za Sektretariati ya
maadili kuwasilisha malalamiko yake.
Naibu waziri wa ofisi ya makamu wa Rais,
Muungano na Mazingira Luhaga Mpina
ambapo amesema kuwa atawahisha
kurudisha fomu hizo kabla ya saa kumi
na mbili jioni.
0 comments :
Post a Comment