Serikalai ya uingereza yaridhishwa na utendaji wa serikal ya awamu ya tano.
erikali ya Uingereza imeeleza kuridhishwa na
utendaji kazi wa rais wa Tanzania Dr John
Pombe Magufuli katika kubana matumizi pia
kupambana na rushwa na kwamba nchi yake iko
tayari kutoa ushirikiano kwa Tanzania katika
kuliimarisha jeshi la polisi na idara ya
mahakama.
Hayo yamesemwa na balozi wa Uingereza hapa
nchini Dianna Melrose alipokutana na kufanya
mazungumzo na rais wa jamhuri ya muungano
wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli Ikulu jijini
Dar es Salaam na kuongeza kuwa waziri mkuu
wa Uingereza David Cameroon anaridhishwa na
hatua zinazochukuliwa na rais John Pombe
Magufuli katika kupambana na rushwa hapa
nchini.
Mbali na balozi huyo wa uingereza hapa nchini
pia rais Dkt John Pombe Magufuli pia amekutana
na kufanya mazungumzo na balozi wa Afrika
Kusini hapa nchini Thamsanqa Mseleku, na kisha
Mh Mohamed Yasserel Shawaf balozi wa Misri
hapa nchini mazungumzo yaliyofanyika Ikulu jijini
Dar es Salaam.
Katika tukio jingine rais Dkt John Pombe
Magufuli amepokea hati za utambulisho za
mabalozi ambapo balozi wa kwanza kuwasili
Ikulu na kukabidhi hati zake ni balozi wa jamhuri
ya kidemokrasia ya Kongo DRC Mh Jean Pierre
tshampanga na kisha kufuatiwa na balozi wa
Namibia Mh Theresia Samaria matukio
yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Aidha, rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania
Dkt John Pombe Magufuli amekutana na kufanya
mazungumzo na rais mstaafu wa awamu ya nne
Dkt Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es
Salaam.chanzo itv.
0 comments :
Post a Comment