Tatizo la ajira afrika na kati chanzo ni rushwa asema makamu wa rais tz.soma zaid.
Makamu wa rais Mhe. Samia Suluhu Hassani
amesema nchni za Afrika Mashariki na kati
zitaweza kuongeza ajira zaidi iwapo zitapunguza
rushwa, urasimu na kuhamisha uwekezaji toka
nje ya nchi kwa kuweka sera nzuri na masharti
nafuu.
Akizungumza na vyombo vya habari katika
ufunguzi wa mkutano wa nane wa kimataifa wa
jumuiya ya shirikisho la mifuko ya hifadhi ya
jamii ya nchi za Afrika Mashariki na kati, Mhe
Samia amelitaka shirikisho hilo kuzisaidia nchi za
Afrika Mashariki na kati kuzalisha ajira na
kusisitiza lengo la Tanzania ni kuingiza sekta
isiyorasmi katika mifumo ya hifadhi ya jamii ili
kuboresha maisha ya watanzania.
Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu, sera bunge,
kazi, ajira, vijana na walemavu Mhe. Jenista
Mhagama amesema kupitia mpango wa kukuza
ajira kwa vijana kwa kushirikisha mifuko ya
hifadhi ya jamii kutaweza kufikiwa lengo la
Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ambapo
pia amewataka watanzania kutokuwa na hofu ya
kufirisika kwa mifuko hiyo kutokana na kujiingiza
katika biashara ya uwekezaji.
0 comments :
Post a Comment