Baraki obama ampa ujasiri castro rais wa cuba kutoiogopa marekani.soma zaid.
Rais wa Marekani Barack Obama ameeleza
matumaini yake kwamba hali ya Cuba
itaimarika, kwenye hotuba iliyopeperushwa moja
kwa moja kupitia runinga.
Kiongozi huyo wa Marekani, ambaye ndiye wa
kwanza kuzuru Cuba akiwa bado madarakani
katika kipindi cha miaka 88, alitoa hotuba hiyo
kutoka ukumbi wa Grand Theatre mjini Havana.
Bw Obama alisema alifika Cuba “kuzika masalio
ya Vita Baridi” na miongo mingi ya uhasama.
Alimwambia Rais wa Cuba Raul Castro kwamba
hafai kuiogopa Marekani na pia hafai kuogopa
“usemi wa watu wa Cuba”.
Obama na Castro wajibizana Cuba
Bw Obama alisema wakati umefika kwa Marekani
na Cuba kuacha nyuma yaliyopita na kusonga
mbele “kama marafiki na majirani na kama
familia, pamoja” kwa siku za usoni zenye ufanisi.
Amewataka raia wa Cuba kuacha nyuma vita vya
kifalsafa na kujieleza sio kwa kupinga Marekani
bali kwa kujieleza wao binafsi ama raia wa Cuba.
"Licha ya siasa hizi zote, watu ni wale wale na
Wacuba ni Wacuba,” alisema.
Aidha, amehimiza kuondolewa kwa vikwazo vya
kibiashara vilivyowekewa nchi hiyo na Marekani
miaka 54 iliyopita. Tamko hilo lilishangiliwa sana
na raia wa Cuba.
Ni Bunge la Congress pekee linaloweza
kuidhinisha kuondolewa kwa vikwazo hivyo.
Bw Obama alikamilisha ziara yake ya siku tatu
kwa kuungana na Rais Castro kutazama mechi
ya besiboli uwanja wa Latinoamericano mjini
Havana.
Tampa Bay Rays waliilaza timu ya taifa ya Cuba
4-1.
Baada ya kuondoka Cuba, Bw Obama ameelekea
Argentina siku ambayo inalingana na
maadhimisho ya miaka 40 tangu kutokea kwa
mapinduzi yaliyoingiza mamlakani utawala
dhalimu wa kijeshi.
Baadhi ya makundi yanapanga maandamano
kushutumu Marekani ambayo inadaiwa kusaidia
jeshi wakati wa mapinduzi hayo ya 1976.chanzo bbc swahil
0 comments :
Post a Comment