Breaking News
Loading...

Advert

Monday, March 28, 2016

Makaya awataka watanzania kuunga mkono jitihada za Rais magufuli.

Askofu wa kanisa la Anglikana Dayosisi ya
Western Tanganyika Kigoma Sadock Makaya
amewataka watanzania kuunga mkono jitihada za
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mh.Dk John Magufuli katika kukabiliana na
uzembe,wizi na matumizi mabaya ya madaraka
yanayosababishia hasara kwa nchi.
Akihubiri katika ibada ya Pasaka kukumbuka
kufufuka kwa yesu kristu katika kijiji cha
Nyumbigwa wilayani Kasulu,Askofu Makaya
amesema uwepo wa wafanyakazi hewa
wanaolipwa na serikali,ufisadi,rushwa
,kutowajibika na matumizi mabaya ya madaraka
miongoni mwa vitu ambavyo Rais Magufuli
anapambana navyo vinakwamisha maendeleo ya
nchi na watu wake, ambapo wamewataka
watanzania kubadilika na kufuata mafundisho ya
mungu.
Aidha katika ibada hiyo kanisa la Anglikana
Nyumbigwa lilitoa msaada wa vyakula na nguo
kwa watu wasiojiweza na wenye ulemavu
mbalimbali,ambapo Askofu Makaya ameeleza nia
ya kanisa hilo Dayosisi ya Western Tanganyika
pamoja na kuhubiri injili ni kusaidia jamii hasa
wahitaji kimwili huku mchungaji Richard Shumbu
wa kanisa hilo akieleza kuwa zaidi ya wahitaji
mia moja wamenufaika na msaada huu.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top