Mashindano ya miss tanzania 2016 yafunguliwa rasimi.soma kwa undani ujue jinsi ya kushiriki.
Mashindano ya Miss Tanzania kwa msimu mpya
wa 2016 yamezinduliwa jijini Dar es Salaam
usiku wa kuamkia jana. Mashindano hayo
yalizinduliwa na Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, baada ya
kufungwa kwa muda kwa mashindano hayo na
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kukiuka
utaratibu na kanuni za kuendesha mashindano
hayo.Akizungumza wakati wa uzinduzi wa
shindano hilo, ambalo limebeba kauli mbiu ya
‘Mrembo na Mazingira Safi’ alisema yeye kama
waziri mwenye dhamana atayaangalia
mashindano hayo kwa umakini mkubwa.“Watanza
nia mrudishe tena imani yenu kwa mashindano
haya na kuhakikisha yanafanyika kwani
madhumuni ni kuibua vipaji na kutengeneza ajira
mbalimbali,” alisema Nnape.
Aidha, Nape aliwataka wasimamizi wa
mashindano hayo yanayoandaliwa na Kampuni ya
Lino International Agency chini ya Mkurugenzi
wake, Hashim Lundenga kuhakikisha
wanayasimamia mashindano hayo na kuzingatia
madhumuni yake.
0 comments :
Post a Comment