Hiki ndo alichokisema shekh ponda juu ya utawala wa maguful.soma zaid.
SHEIKH Ponda Issa Ponda, Katibu wa
Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania,
amekosoa utendaji wa Rais John
Magufuli, hasa dhana ya kutumbua
majipu, akisema ina kasoro za kiutawala.
Akizungumza leo, Sheikh Ponda amesema
utendaji wa Rais Magufuli ni wa
kulipualipua.
“Ni kweli kwenye serikali kulikuwa na
matatizo mengi, lakini lazima utaratibu
kamili wa kuchukulia watu hatua ufuatwe,”
amesema na kuongeza:
“Huwezi kuchukulia hatua watu bila kuwa
na ripoti ya kitaalamu. Huko ni kufanya
kazi kwa kulipuka.
Watanzania watafurahi zaidi kama serikali
haitaingia hasara kutokana na kazi hiyo
iliyo na shaka katika utekelezaji wake.”
Amesema ingekuwa bora kwa Rais
Magufuli kusubiri ripoti za wataalamu
wake, na si ‘kutumbua majipu’ kabla ya
kupata ripoti.
Anasisitiza, “Jambo hili halipo sawa hata
kidogo.”
Anasema dhamira ya kurejesha nidhamu
serikalini ni nzuri na inahitajika sana,
lakini namna ya utekelezaji wa dhamira
yake hakuuanza vizuri.
“Juzi Rais Magufuli amepokea ripoti
kutoka kwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali. Angepaswa kuanza kuifanyia kazi
ripoti hiyo ili kuepuka madhara kama yale
ya kukamata meli ya uvuvi kwenye Pwani
ya Dar es Salaam mwishowe serikali
ikaingia gharama,” amesema Sheikh
Ponda.
0 comments :
Post a Comment