Kudhoofika kiafya kwa huyu mrembo kumesababisha asionekane kwenye matangazo uingereza.soma zaid.
Kampuni ya Gucci imepigwa marufuku kutumia
tangazo moja nchini Uingereza ambalo
linamuonyesha modela mmoja aliyedhoofika
kiafya.
Mamlaka ya viwango vya matangazo imeamua
kwamba vile alivyosimama mwanamke huyo
pamoja na alivyojipodoa kunamuweka aonekane
kama aliyeathirika kutokana na ukosefu wa mlo.
Gucci iliitetea picha hiyo ikisema kuwa iliwalenga
watu wazima na kusisitiza kuwa mwanamitindo
huyo alikuwa mwembamba tu.
Lakini tangazo hilo haliwezi kutumika tena hadi
litakapofanyiwa marekebisho.
Mamlaka hiyo imesema kuwa ilibaini kwamba
kiwiliwili cha mwanamitindo huyo pamoja na
mikono yake ilikuwa myembamba na haikuwa
sawa na kichwa na eneo la chini la mwili wake.
''Pia tulibaini kwamba hisia za uso wake na
vipodozi vyake vyeusi alivyopakwa hususan
kandokando ya macho yake vinamfanya
kuonekana aliyedhoofika.Kwa sababu hizo
tumeamua kwamba mwanamitindo huyo
aliyekuwa anategemea ukuta amedhoofika kiafya
na kwamba tangazo hilo halina uwajibikaji''.
Wanaharakati wanasema kuwa mwanamitindo
huyo wambemba kupitia kiasi wanaweza kuharibu
kujiamini kwa wanawake na wasichana kupitia
ukuzaji maumbile yalioathirika kiafya .chanzo bbc swahili.
0 comments :
Post a Comment