Kutoka bungeni# waziri mkuu elimu ni nguzo mhimu katika maendeleo ya taifa na jamii kwa ujumla.soma zaid.
Bunge la 11 limeendelea tena leo April 22 2016,
Waziri mkuu Kassim Majaliwa amehutubia bunge
kuhusu mapitio na mwelekeo wa kazi za Serikali
na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za
ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka 2016/2017.
Katika kitengo cha huduma ya Jamii Elimu,
Waziri Majaliwa amesema ‘ Kwa kutambua
umuhimu wa Elimu kama nyenzo imara ya
maendeleo ya kiuchumi na kijamii, Serikali imeanza
kuboresha na kuimarisha elimu ya awali, msingi,
sekondari, ufundi na elimu ya juu.’
‘ Baada ya kuanza utekelezaji wa mpango wa elimu
bila malipo, kumejitokeza changamoto kadhaa,
ikiwemo miundombinu kama madarasa, mabweni,
maabara, nyumba za walimu na vyoo ‘ ;-Waziri
Mkuu Majaliwa
‘ Napenda kuwahakikishia wananchi kwamba
Serikali inaendelea kuzifanyia kazi changamoto
hizo na jitihada kubwa zimewekwa‘ ;-Waziri Mkuu
Majaliwa
‘ Nitumie nafasi hii kuwashukuru wadau walioanza
kuchangia madawati katika maeneo mbalimbali,na
niwasihi wengine waendelee kuunga mkono Serikali
yao ‘ ;- Waziri Mkuu Majaliwa
‘ Kuanzia leo hii, nawaagiza Wakuu wa Wilaya na
Wakurugenzi wote waliokamata mbao ndani ya
Halmashauri zao kuzitumia kutengeneza madawati
na siyo kuzipiga mnada ‘ ;-Waziri Mkuu Majaliwa
‘ Hali ya urejeshaji wa mikopo iliyotolewa
hairidhishi, Hivyo naagiza Bodi ya mikopo ya Elimu
ya Juu kufuatilia urejeshaji wa mikopo hiyo ili
fedha hizo zitumike kuwakopesha wanafunzi
wengine‘ ;-Waziri Mkuu Majaliwa
0 comments :
Post a Comment