Breaking News
Loading...

Advert

Tuesday, April 5, 2016

Mkoa wa mwanza kuhakiki tena upya watumishi hewa kwa kutumia picha na finga za vidole.


Mwanza. Baada ya kuongoza kitaifa kwa kuwa na
idadi kubwa ya wafanyakazi hewa, uongozi wa
Mkoa wa Mwanza umeamua kuhakiki upya
majina ya watumishi kupitia picha, hati za malipo
ya mishahara na alama za vidole.
Mkuu wa mkoa huo, John Mongella amesema
kuwa uhakiki huo utafanyika kwa siku saba
kwenye halmashauri saba za mkoa huo
ulioongoza nchini kwa kuwa na wafanyakazi
hewa 334.
“Katika awamu hii, tume maalumu itakutana na
mfanyakazi mmoja mmoja kuchukua picha zao,
hati zao za malipo ya mishahara na kuchukua
alama zao za vidole, “Baada ya zoezi hilo suala
la wafanyakazi hewa litabaki kuwa historia
mkoani Mwanza,” amesema Mongella.
Amesema tayari majina ya wafanyakazi hewa
129 waliobainika katika orodha ya watu 334
yamefutwa kutoka kwenye orodha ya
kumbukumbu baada ya Serikali kujua waliko,
huku uchunguzi ukiendelea kuwabaini 205
waliosalia.
Amesema uchunguzi wa awali unaonyesha mkoa
huo una idadi kubwa ya watumishi hewa, hasa
katika idara ya elimu ambayo uajiri walimu wengi
na kuripoti vituo vya kazi kisha kutokomea
kusikojulikana huku wakiendelea kulipwa
mishahara na Serikali.
“Wapo walimu walioajiriwa na kuripoti shuleni,
lakini wakaamua kuendelea na masomo au
kupata ajira maeneo mengine, ila majina yao
bado yako kwenye orodha ya watumishi
wakiendelea kulipwa mishahara. Hawa
tutawabaini katika zoezi linaloendelea,” amesema
Mongella.
Ameonya kuwa Serikali itawachukulia hatua
watendaji wote watakaobainika kuhusika
kupitisha malipo ya mishahara hewa huku
wakijua wahusika hawapo kazini.
Pamoja na kushughulikia na kudhibiti matukio ya
uhalifu na migogoro ya ardhi katika maeneo yao,
Rais John Magufuli aliwaagiza wakuu wapya wa
mikoa siku alipowaapisha kuchunguza, kubaini na
kuwasilisha ofisini kwake idadi ya wafanyakazi
hewa katika mikoa yao ili kudhibiti upotevu wa
fedha za umma.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top