Sakata la lugumi ineterprises vigogo wahaha.soma zaid.
*Milioni 500/- hazijulikani zilizopo, zabuni yake
ilitangazwa siku moja
*Taarifa ya polisi, CAG zatofautiana, kamati
yaahidi kumuona Spika
DODOMA
WAKATI sakata la ufisadi wa mkataba kati ya
Kampuni ya Lugumi Enterprises Ltd na Jeshi la
Polisi likiendelea kufukuta, imebainika Sh milioni
500 zilichotwa bila maelezo yoyote.
Habari za uhakika zilizopatikana mjini hapa jana,
zinasema upotevu huo umebainika baada ya
Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali
(CGA), kufanya ukaguzi wa taarifa za mapato na
matumizi ndani ya Jeshi la Polisi.
Taarifa hizo ziliwasilishwa juzi na Ofisa Masuhuli
wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Meja Jenerali Projest Rwegasira na Naibu
Inspekta Generali wa Polisi (D/IGP),
Abdulrahman Kaniki.
Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika kutoka
ndani ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali
(PAC), vigogo hao walishindwa kutoa maelezo ya
kina kuhusu tofauti hiyo ya fedha, mbele ya
wajumbe wa kamati hiyo.
Chanzo hicho kiliiambia MTANZANIA mjini hapa
jana, kuwa wajumbe wote walitilia shaka
mkataba kati ya polisi na Kampuni ya Lugumi
ambao zabuni yake ilitangazwa kwa siku moja na
kesho yake ukasainiwa.
YALIYOBAINIKA
Chanzo chetu kinasema katika kikao na vigogo
hao, wajumbe wa PAC walihoji taarifa ya
utekelezaji wa mkataba huo na kuonyesha hofu
ya kuwapo ‘wingu la ufisadi’ ambalo linahitaji
majibu.
“Zabuni ilitangazwa Septemba 22, mwaka 2011
na mkataba kusainiwa Septemba 23, mwaka huo
huo, ndani ya siku moja mkataba ukasainiwa
jambo ambalo ni hatari.
“Jambo jingine linaloshtua, tangu wakati huo
mashine zote wanasema zipo, lakini hazifanyi
kazi na swali ambalo wajumbe wanahoji,
inakuwaje wanatoa zabuni bila kufanya ‘visibility
study’ ya kina ili kujua uwezo wa hii Kampuni ya
Lugumi kama ilishawahi kufanya kazi ya aina hii
ama la.
“Tumejipanga kwa kila hatua, tumemtaka
Makamu Mwenyekiti wetu Aeshi Hilaly,
awasilishe taarifa nzima kwa Spika wa Bunge,
Job Ndugai na mwishowe taarifa hii iwasilishwe
mbele ya Bunge ili umma ujue namna watu
wanavyotafuta fedha kinyume cha sheria,”
kilisema chanzo chetu.
Mbali na hilo, pia kamati imebaini tofauti ya
fedha zilizopo katika mkataba huo ambapo taarifa
ya Jeshi la Polisi inaonyesha walitoa Sh bilioni
37,163,940,127.7, wakati taarifa ya CAG,
inaonyesha zilizotolewa ni Sh bilioni
37,742,913,007, ikiwa na tofauti ya zaidi ya Sh
milioni 500.
“Katibu Mkuu na wenzake, walipotakiwa kutoa
maelezo ya kina kuhusu zilipo Sh milioni 500
walishindwa, wajumbe wakageuka mbogo na
kutaka suala hilo litolewe maelezo ya kina.
“Licha ya hali hii, PAC tulibaki tukijiuliza, hata
kama kulikuwa na ulazima wa kufunga mashine
hizi kwa dharura inakuwaje hazifanyi kazi?
Maana kuna kila dalili ya fedha za umma kuliwa
mchana kweupe,” kilisema chanzo chetu.
Pia kamati hiyo ilibani mkataba ulitolewa kwa
‘single source’ (yaani kampuni moja bila
kuishindanisha na nyingine), badala ya tenda
kushindaniwa na kampuni nyingi zaidi.
VIGOGO WAHAHA
Baada ya PAC kuendelea na kazi ya kuchambua
taarifa hiyo, kigogo mmoja ambaye anatajwa
kuhusika katika mkataba huo, amekuwa akihaha
kuomba nguvu ya wabunge wa Kambi ya
Upinzani, hasa wale wanaotokana na vyama
vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi
(Ukawa) ili wamnusuru.
“Ninamshangaa huyo waziri (jina linahifadhiwa),
anahangaika bure, eti anasema watu
hawampendi na wanamchukia, amefikia hatua ya
kusema PAC inatumiwa na wauza dawa za
kulevya.
“Sisi ni wajumbe ambao kila mmoja anajiweza,
hata siku moja hatuwezi kukaa kutegemea fedha
za watu, ila tunafanya kazi kwa masilahi ya nchi
yetu na si vinginevyo. Tumeridhika na posho
tunazolipwa na Bunge, hatuna haja ya kutumika
kwa mtu yeyote ila tunasukumwa na uzalendo
kwa Taifa letu,” kilisema chanzo chetu.
Katika kile kinachoonekana ni kama maigizo,
baada ya PAC kutaka mkataba na taarifa ya
utekelezaji wa mradi huo wa ufungaji wa
mashine za utambuzi wa alama za vidole katika
vituo vya polisi 108 nchini, sakata hilo limekuwa
likichukua sura mpya kila kukicha.
Uamuzi huo uliibua hisia miongoni mwa jamii
ambapo katika kipindi cha siku mbili baada ya
PAC kutaka ripoti hiyo, Kamati ya Bunge ya
Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, iliingilia kati
ambapo mwenyekiti wake, Balozi Adadi Rajabu,
alikiri kupokea mkataba huo.
UTATA
Kampuni ya Lugumi inadaiwa kupewa tenda na
jeshi hilo kwa ajili ya kufunga mashine za
kuchukua alama za vidole – ‘Biometric Access’
katika vituo 108 nchi nzima kwa gharama ya Sh
bilioni 37.
Hadi sasa mashine hizo zimefungwa katika vituo
14 pekee na tayari kampuni hiyo imelipwa Sh
bilioni 34 ambazo ni sawa na asilimia 99 ya
fedha zote za mkataba.
Katika sakata hilo, inadaiwa Kampuni ya Lugumi
ilipewa zabuni hiyo ikiwa haina uzoefu wa kazi
hiyo.
“Wamepewa mkataba sawa, lakini mbona taarifa
zinaonyesha kuwa kampuni hii haijasajiliwa kama
Biometric Access Company na haijawahi kufanya
kazi zozote zinazohusu Biometric Access
Control?” alihoji mmoja wa wataalamu.
Chamxo mtanzania
0 comments :
Post a Comment