TUCTA yapendekeza kima cha chini cha mshahara kwa wafanyakazi sh.750,000.soma zaid.
Serikali ya Tanzania imetakiwa kushusha
kiwango cha kodi kinachokatwa kwenye
mishahara ya wafanyakazi sambamba na
kupandisha kima cha chini cha mshahara
kufikia 750,000 ili kuweza kuboresha
maisha ya wafanyakazi.
Katibu mkuu wa shirikisho la vyama vya
wafanyakazi nchini TUCTA Bwana
Nicholous Mgaya amesema wafanyakazi
wengi wanaishi katika mazingira magumu
kutokana na kipato kidogo wanachopata
huku wakizungukwa na kero nyingi
kutoka kwa waajiri wao ikiwemo kulipwa
mishahara kidogo.
Mgaya amesema ni vyema serikali katika
awamu hii ya tano ihakikishe kuwa sera
ya uboreshwaji mishahara inaundwa ili
kuweza kuwadhibiti waajiri ambao
wanashindwa kufuata sheria na taratibu
za ajira.
Mgaya pia amekemea suala la raia wengi
wa kigeni kuweza kupewa ajira kwa wingi
katika maeneo ya migodi, hoteli zenye
hadhi ya kimataifa, viwandani na kwenye
shule binafsi na kutaka msako wa
kuwaondoa uendelee ili fursa za ajira
ziwafikie watanzania.
0 comments :
Post a Comment