Breaking News
Loading...

Advert

Monday, May 30, 2016

# Dodoma Bungeni hapatoshi wabunge wa ukawa watoka nje bunge limeahirishwa

BUNGE la Tanzania limeahirishwa. Ni kutokana
na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa) kugomewa kuwasilisha hoja
binafsi kuhusu wanafunzi wa Chuo Kikuu cha
Dodoma (UDOM) kusimamishwa, anaandika Faki
Sosi.

Hatua hiyo imetokana na Tulia Ackson, Naibu
Spika kugomea mwongozo uliotolewa na
mbunge kutoka Ukawa kuhusu kujadiliwa
taarifa ya kusimamishwa kwa wanafunzo
kutoka chuo hiko.
Taarifa kutoka bungeni zinaeleza kwamba,
Ackson aligomea taarifa hiyo jambo limezua
mzozo na hatimaye wabunge kuamua kutoka nje
ikiwa ni ishara ya kutoridhika na uamuzi wa kiti
cha spika. Mwanahalisi Online linaendelea
kufuatilia.
Juzi Udom kilitoa taarifa ya kusimamisha
masomo zaidi ya wanafunzi 7,000 wa kozi
maalumu ya ualimu wa Sayansi, Hisabati na
Teknolojia kwa ngazi ya Stashahada na kisha
kutaka waondoke chuoni hapo mara moja.
Tangazo hilo liliwataka wanafunzi hao kuondoka
kati ya juzi na jana saa 12 jioni. Tangazo hilo
lilieleza kuwa kutokana na matatizo yaliyopo
katika ufundishaji wa stashahada hiyo, Serikali
kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na
Mafunzo ya Ufundi imeamua wanafunzi hao
kurejea majumbani na kwamba wataelezwa
mustakabali wao “mapema iwezekanavyo”.
Kozi ya Stashahada ya Ualimu wa Sayansi,
ilianzishwa maalumu kwa agizo la Rais Mstaafu,
Jakaya Kikwete kwa lengo la kuziba pengo la
walimu wa sayansi na ilikuwa inatolewa UDOM
pekee.
Waliokuwa na sifa za kujiunga na kupewa mikopo
ni wanafunzi waliomaliza kidato cha nne na
kufaulu vizuri masomo ya sayansi.
Wanafunzi hao waliokuwa wamekopeshwa na
serikali wamesimamishwa siku mbili baada ya
wenzao zaidi ya 480 wa Chuo Kikuu cha St.
Joseph kusimamishwa baada ya kubainika
kutokuwa na sifa za kudahiliwa.chanzo meanahalisonline.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top