Breaking News
Loading...

Advert

Sunday, May 29, 2016

Kampuni ya Dangote imetangaza kushusha bei ya saruji yake.soma zaid.


Kampuni ya saruji ya Dangote imetangaza bei ya
saruji yake kuwa itakuwa Sh 10,000 popote, ikiwa
ni punguzo.
Imesema punguzo hilo linalenga kuongeza
ushindani kwenye soko la bidhaa hiyo nchini na
kuwezesha watanzania wengi kununua
saruji.Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo,
SadaLadan-Baki, alisema bei ya saruji yao aina
ya 32.5R itauzwa bei hiyo ya Sh 10,000 kwa
mfuko wa kilo 50; na saruji ya 42.5R itauzwa Sh
10,500 kwa mfuko wa kilo 50 kutoka kiwandani
mpaka popote itakapouzwa, ikiwemo jijini Dar es
Salaam, ambako bidhaa hiyo inapatikana.Hatua
hii imetajwa kuwa inafanya saruji ya Dangote
kuwa ya bei nafuu kuliko nyingine, ambazo
zinauzwa kati ya Sh 12,500 na Sh 14,000 jijini
Dar es Salaam.Sada alisema hatua hiyo itasaidia
maendeleo ya miundombinu na kutilia mkazo
mpango wa taifa wa kukabili tatizo la makazi
nchini kutokana na takwimu kuonesha hapa
nchini upo uhaba wa nyumba milioni
tatu.“Tunatambua uhitaji mkubwa wa miundo
mbinu bora, na moja ya njia ya kulikabili tatizo
hili ni kumfanya kila mtanzania kuweza kuwa na
uwezo wa kununua rasilimali za ujenzi kwa
kuweka bei mbadala kwa kila Mtanzania,”
alisema Sada.
Uongozi huo wa kampuni ulisema bei hiyo elekezi
kati ya Sh 10,000 na 10,500 imelenga jijini Dar es
Salaam, ambako ndiko kitovu cha biashara,
kinachoangaliwa na wafanyabiashara kutoka
maeneo mbalimbali.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top