Breaking News
Loading...

Advert

Tuesday, May 24, 2016

Kutoka zanzibar hatutishwi na misaada ya wahisani.soma zaid


BAADHI ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi
wameitaka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
kutobabaishwa na baadhi ya washirika wa
maendeleo waliotishia kususa misaada kwa
malengo ya kisiasa.
Wamesema kwa nyakati tofauti katika vikao vya
baraza hilo vinavyoendelea mjini hapa kuwa, ni
bora kula mihogo na sembe kuliko kupokea
misaada yenye masharti ya kudhalilisha.
Mwakilishi wa Uzini, Mohamed Raza (CCM)
alisema hatua ya kusitishiwa misaada kutoka
nchi washirika wa maendeleo kwa Zanzibar si
mara ya kwanza.
Alikumbusha kuwa wakati wa uongozi wa Rais Dk
Salmin Amour (Komandoo) mara baada ya
kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa kwanza wa
mfumo wa vyama vingi mwaka 1995, suala hilo
lilitokea.
Alisema Dk Amour alizuiliwa misaada kutokana
na washiriki wa maendeleo kutokubaliana na
Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 uliofanyika kwa
madai kwamba haukuwa huru na haki ambapo
CUF ilishindwa na CCM.
“Mwaka 1995 mara baada ya kumalizika kwa
uchaguzi mkuu wa kwanza wa mfumo wa vyama
vingi Dk Salmin aliwekewa vikwazo na nchi
washiriki wa maendeleo kwa madai kwamba
uchaguzi haukuwa huru na haki. Lakini nchi
ilikwenda na kutekeleza miradi yake yote ya
ndani kwa kutumia rasilimali zake,” alifafanua
Raza.
Akitoa mfano, Raza alisema katika kipindi hicho
miradi ya ujenzi wa nyumba za maendeleo
zilizopo Michenzani ulifanyika na kukamilika kwa
ghorofa moja lililopo jirani na kituo cha Polisi
Madema kwa kutumia fedha za ndani
zinazotokana na makusanyo ya kodi.
Naye Mwakilisi wa Tunguu, Simai Mohamed Said
alisema huu ni wakati muafaka kwa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar kujikita zaidi katika
kutumia rasilimali zake kwa ajili ya kuongeza
pato la taifa. Alisema taasisi zinazoshughulikia
utalii hawajaitangaza vizuri Zanzibar katika
ramani ya dunia, kwa hivyo sekta hiyo
haijatumiwa vizuri katika kuingiza pato la taifa.
Alisema sekta ya utalii inaingiza fedha za kigeni
kwa asilimia 46 na pato la taifa kwa asilimia 68
kwa hivyo ni wajibu wa taasisi zinazoshughulikia
kuitangaza Zanzibar kufanya kazi hiyo kwa
kutumia matamasha ya nje ya kimataifa.
“Miongoni mwa njia za kuifanya Zanzibar
kujitegemea na kuacha kupiga magoti kwa
washiriki wa maendeleo ni kutumia rasilimali
zake za ndani ikiwemo sekta ya utalii ambayo ni
tegemeo katika kuingiza fedha za kigeni,”
alisema Raza.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top